Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Bakari Machumu (kulia) baada kuwasili makao makuu ya MCL jijini Dar es Salaam leo. Nape ni mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mwonekano mpya wa tovuti za kampuni za Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ambazo sasa zinapatikana kwa njia rahisi kwa mtumiaji kuona habari mpya. Picha na Edwin Mjwahuzi