Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan jana Alhamisi, Oktoba 31, 2024 amekutana na kuzunguma na Naibu Kiongozi Mkuu wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Isobel Coleman, Iowa nchini Marekani.
Oktoba 30, 2024, Rais Samia alishiriki mjadala kuhusu kilimo barani Afrika, katika mji wa Des Moines, Iowa nchini humo.
Mjadala huo uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, serikali na sekta binafsi Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo. Picha na Ikulu