Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) jijini Moscow, Russia, huku akisema heshima hiyo si ya mafanikio yake binafsi bali ni utambuzi wa mchango wa Watanzania wote katika maendeleo ya Taifa na ushirikiano wa kimataifa.
Shahada hiyo ametunukiwa Juni 4, 2026, wakati wa ziara yake ya kitaifa nchini Russia, ambapo uongozi wake, mchango katika maendeleo ya kijamii, mageuzi ya elimu na diplomasia ya kimataifa vimetajwa kuwa sababu za kutambuliwa kwake.