Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hanlink Mobility: Gwiji wa usafirishaji Afrika Mashariki atua Tanzania, aahidi mapinduzi ya viwanda na ajira

Katika ulimwengu wa biashara ya kisasa, usafirishaji ndiyo uti wa mgongo wa uchumi. Bila mifumo madhubuti ya ubebaji mizigo na mitambo imara, gurudumu la maendeleo ya viwanda hukwama.

Ni katika muktadha huu, Jiji la Dar es Salaam mnamo Juni 26, 2026, lilishuhudia tukio la kihistoria ambalo limebadili kabisa ramani ya uwekezaji katika sekta ya magari na mit ambo nchini Tanzania.

Kampuni ya Hanlink Mobility Tanzania ambayo ni mwanachama wa Kundi la Makampuni ya Hanlink (Hanlink Group), ilizindua rasmi shu ghuli zake kama msambazaji aliyeidhinishwa wa magari ya chapa maarufu duniani ya SINOTRUK.

Uzinduzi huu haukuwa tu ufunguzi wa kituo kipya cha mauzo (showroom) chenye teknolojia ya kisasa, bali ni tamko la wazi kuwa Tanza nia sasa imekuwa kitovu cha kimkakati cha kampuni hiyo katika upanuzi wake barani Afrika.


Safari ya matumaini: Kutoka Uganda hadi Tanzania

Hanlink Mobility si jina geni katika anga la usafirishaji Afrika Mashariki. Safari yake ilianzia nchini Uganda kupitia kampuni ya Double Q Company Limited, ambapo ilijijengea heshima kabla ya kutanua mbawa zake kwa mafanikio nchini Rwanda, Kenya, Sudan Kusini, na Jamhuri ya Kide mokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza kwa hisia kali wakati wa hafla ya uzin duzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Han link Mobility Group, Lin Yu alisisitiza kuwa uamuzi wa kuwekeza nchini Tanzania ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi hii.

“Upanuzi wetu unaonyesha imani tuliyonayo kwa Afrika Mashariki na dhamira yetu ya kuchangia maendeleo yake,” alisema Yu.

Aliongeza kuwa, kuingia Tanzania si tu kwa ajili ya kuongeza orodha ya nchi walizozifikia, bali ni kuimarisha mtandao wa kikanda ambao utawapa wateja uhakika wa kupata huduma popote wali po katika nchi sita walizopo mpaka sasa.


Ahadi ya kukuza shughuli za viwanda na ajira kwa Watanzania

Moja ya mambo yaliyowavutia wadau wengi ni maono ya Hanlink Mobility zaidi ya kuuza malori. Yu alifichua kuwa, kampuni hiyo tayari imewekeza katika kiwanda cha kisasa cha kuunganisha magari (assembly plant) nchini Uganda, hatua iliyozalisha ajira nyingi na kusaidia kuongeza wa ujuzi kwa wazawa.

“Tuna shauku ya kutekele za miradi kama hiyo ya kuunganisha magari hapa Tanzania katika siku zijazo. Tunaamini hili litaongeza fursa za ajira na kuimarisha sekta ya viwanda nchini,” ali sisitiza Yu.

Hii ni habari njema kwa vijana wa Kitanzania ambao wanahitaji fursa za kujifunza teknolojia ya kisasa ya uten genezaji wa magari makub wa. Zaidi ya malori ni suluhisho la ‘vifaa vyote chini ya paa moja.’

Sifa nyingine inayofanya Hanlink Mobility kuwa kimbilio la wafanyabiashara ni uwezo wake wa kutoa huduma mtambuka.

Meneja Mkuu Msaidizi wa Hanlink Mobility Tanzania, Bi. Zainab Ngoda alifafanua kuwa kampuni hiyo imejipambanua kama mtoa huduma jumuishi wa usafiri na vifaa vya viwandani na migodini.

Mbali na SINOTRUK, Hanlink inawakilisha bidhaa nyingine za daraja la kwanza duniani kama mitambo ya ujenzi wa barabara na migo dini ya XCMG, ‘forklifts’ za Heli, na mabasi ya Kinglong.

Hii inamaanisha kuwa mkandarasi wa ujenzi au mmiliki wa mgodi anaweza kupata mahitaji yake yote kuanzia malori ya kumwaga mchanga hadi mitambo ya kuchimba madini katika sehemu moja.

Katika ishara ya kuonye sha uwezo wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Bi. Zainab Ngoda aliwatambulisha wafanyakazi wote Hanlink Mobility Tanzania huku akisisitiza kuwa “Nyuma ya mafanikio ya cha pa hizi kubwa kuna timu ya wataalamu wazalendo walio jitolea kuwahudumia wateja wetu kila siku.”

Kama inavyofahamika kuwa, sekta za ujenzi, uchu kuzi, na madini nchini zina hitaji magari yanayostahimili mazingira magumu.

Mkuru genzi wa Mauzo wa Hanlink Mobility Tanzania, Peter Li alieleza kuhusu magari ambayo yametengenezwa kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kukidhi mahitaji hayo.

Baadhi ya bidhaa zilizo ingizwa sokoni na kampuni hiyo ni pamoja na: Malori ya mchanga (Tippers): HOWO H3 (4x2) na HOWO TX (6x4) ambayo ni mahususi kwa ujenzi na shughuli za migo dini.

Vichwa vya Trela (Tractor Heads): HOWO NX na HOWO MAX, vilivyoundwa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo ya masafa marefu ndani na njeya mipaka ya Tanzania. Malori Mepesi (Light Duty Trucks): Yenye uwezo wa kubeba tani 3, 5, 8 hadi 10, yakilenga biashara za usam bazaji kwa wajasiriamali wadogo.

Li alisisitiza kuwa “Uhusiano wetu na mteja unaanza baada ya mauzo. Tunatoa dhamana ya kifaa ama mtambo, vipuri halisi na mafundi waliobobea ili kuhakikisha gari linakaa barabarani na kuingiza faida.”


Suluhisho la mitaji kwa wafanyabiashara

Changamoto ya mtaji imekuwa ikiwarudisha nyuma wafanyabiashara wengi. Kwa kulitambua hilo, Mkuu wa Masoko wa Hanlink Mobility Group, Musani Richard, alitangaza ushirikiano wa kimkakati kati ya kampuni hiyo na benki kubwa nchini.

Alisema Hanlink inashirikiana na benki za CRDB, NBC, NMB, na NCBA ili kutoa mikopo nafuu na mipango ya kifedha inayoweza kumlipa mteja kulingana na mzunguko wa biashara yake.

“Tunataka kufanya umiliki wa magari na mitambo mizito kuwa rahisi. Kupitia ushirikiano huu, wafanyabiashara na wajasiriamali wanaweza kupata vifaa wanavyohitaji bila mzigo mkubwa wa mtaji wa awali," alisema Richard. Kutokana na ukuaji wa teknolojia, Hanlink Mobility pia imewekeza kwenye teknolojia ya kidijitali ili kurahisisha mawasiliano.

Katika hafla hiyo Richard aliitambulisha tovuti mpya (www.hanlink.com/tz) na kurasa za mitandao ya kijamii kama Facebook, TikTok, na LinkedIn.

“Mteja anaweza kupata taarifa za bidhaa, ushauri wa kiufundi na msaada wa haraka kupitia simu yake bila kulazimika kufika ofisini.” alieleza

Hii inaenda sambamba na kaulimbiu yao ya "Kutoka Dar hadi Kila Maili" (From Dar to Every Mile), ambayo ni ahadi ya kuwa karibu na mteja iwe yuko bandarini Dar es Salaam, migodini Geita, au kwenye miradi ya ujenzi nchini.

Uzinduzi wa Hanlink Mobility nchini Tanzania unakuja katika kipindi mwafaka ambacho nchi ipo kwenye kasi ya ujenzi wa miundombinu, kuimarisha sekta ya madini na kukuza biashara ya kikanda.

Kwa kuleta bidhaa za SINOTRUK zenye ubora wa kimataifa, huduma bora baa da ya mauzo, na urahisi wa kupata mikopo, Hanlink imejiweka nafasi ya kuwa zaidi ya msambazaji bali mshirika wa maendeleo ya kiuchumi.

Kama alivyosema Yu, huu ni mwanzo wa ukurasa mpya. Hanlink Mobility Tanzania sasa iko hapa kuwapa Watanzania nguvu ya kusonga mbele, maili baada ya maili, huku ikijenga msingi wa Tanzania ya viwanda na mafanikio ya kibiashara.