Watu Credit (Tanzania) Limited yaadhimisha miaka mitano ya ujumuishaji wa kifedha, ikiwezesha mikopo ya zaidi ya Sh 700 bilioni
Mdahalo mkubwa ukiendelea wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya Watu Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa Superdome, Masaki, Dar es Salaam. Mdahalo huo uliangazia safari ya miaka mitano ya kupanua fursa Tanzania kupitia huduma za usafiri, mawasiliano, teknolojia, umiliki wa mali na ushirikiano wa kimkakati, huku ukibainisha ukuaji wa Watu Tanzania, nguvu ya ushirikiano wake na mchango wake katika kuimarisha huduma za usafiri, mawasiliano na fursa za kujipatia kipato kwa Watanzania. Kutoka kushoto ni; Muongoza Mdahalo, Khalila Mbowe, Meneja Mkaazi wa Watu Tanzania, Rumisho Shikonyi (wa pili kushoto) Meneja Mkuu wa Uendeshaji, Watu Tanzania, Abdallah Mohamed (katikati), Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa Watu Group, Erick Massawe (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za simu, Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga (kulia). Hafla hii ilifanyika Juni 29, 2026, jijini Dar es Salaam.
Watu Credit (Tanzania) Limited yaadhimisha miaka mitano ya ujumuishaji wa kifedha, ikiwezesha mikopo ya zaidi ya Sh 700 bilioni
Watu Credit (Tanzania) Limited imeadhimisha miaka mitano tangu kuanza shughuli zake nchini Tanzania, ambapo hadi sasa imehudumia zaidi ya wateja milioni moja na kupanua huduma zake hadi kufikia mikoa 26 kote nchini.
Tangu kuanzishwa kwake jijini Dar es Salaam mwaka 2021, Watu Credit Tanzania imewezesha ununuzi wa pikipiki na bajaji zaidi ya 70,000 na simu janja zaidi ya milioni 1.5, ikitoa zaidi ya Sh 700 bilioni kwa ajili ya kuimarisha usafiri, mawasiliano, ujasiriamali na kuongeza kipato kwa wananchi.
Naibu Meneja Mkaazi wa Anayesimamia Mikopo wa Watu Credit Tanzania, Eddsteve Mwangalimi (kushoto), Mkuu wa Idara ya Fedha wa Watu Credit Tanzania, Anastasija Matvejaveja (wa pili kushoto), Meneja Mkaazi wa Watu Tanzania, Rumisho Shikonyi (wa tatu kushoto); Mwenyekiti wa Bodi ya Watu Group, Bhavin Parmar (wa nne kushoto); Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu wa Watu Credit Tanzania, Anna Linza (wa nne kulia), Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Watu Group, Andrii Volokha (wa tatu kulia), Naibu Meneja Mkaazi Anayesimamia Biashara wa Watu Credit Tanzania, Seuri Kuoko (wa pili kulia) na Mkuu wa Mawasiliano wa Watu Credit Tanzania, Moses Mtweve (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Watu Tanzania iliyofanyika Juni 29, 2026 jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho ya miaka mitano ya Watu Credit Tanzania yalifanyika jijini Dar es Salaam chini ya Kaulimbiu "Kila Mtu Ni Watu," na kuwakutanisha viongozi wa Serikali, washirika wa maendeleo, wateja, wadau wa biashara, wanahabari na wafanyakazi wa Watu Tanzania ambapo kwa pamoja walitafakari mchango wa kampuni hii katika kuboresha maisha ya Watanzania.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Watu Credit Tanzania Rumisho Shikonyi, alisema mafanikio haya yanadhihirisha dhamira ya dhati ya kampuni ya kufikisha huduma na fursa za kifedha kwa Watanzania wengi zaidi.
Ofisa Mkuu wa Masoko, Karimjee Group, Cobus Van Zyl (kushoto), Naibu Meneja Mkaazi wa Watu Credit Tanzania, Seuri Kuoko (katikati) na Mkurugenzi wa Karimjee Group, Amit Singh (kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakionesha ishara ya namba “5” wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya Watu Tanzania. Tukio hilo linaakisi safari ya miaka mitano ya Watu Tanzania katika kupanua upatikanaji wa huduma za usafiri, mawasiliano na fursa za kifedha.
"Miaka mitano iliyopita, Watu Tanzania ilianza ikiwa na imani moja rahisi kwamba, upatikanaji wa fursa haupaswi kutatizwa na ukosefu ama uhaba wa huduma za kifedha. Leo, imani hiyo imekuwa dhahiri na sasa imegeuka kuwa biashara ya kitaifa inayohudumia wateja kote Tanzania na kuwawezesha watu wengi zaidi kupata nyenzo wanazohitaji kwa ajili ya uzalishaji, kuwasiliana na kujenga maisha bora," alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Watu Credit Tanzania Bhavin Parmar, alisema miaka mitano ya kwanza ya kampuni hii imeweka msingi imara wa ukuaji endelevu unaozingatia uwajibikaji.
“Kama Bodi, tunajivunia mafanikio ambayo Watu Credit Tanzania imeyapata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ukuaji huu unaambatana na wajibu, na ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa ubunifu unaendana na uwajibikaji, malengo makubwa yanaongozwa na uadilifu, na kila uamuzi unaongeza thamani ya kudumia wateja wetu, washirika, wafanyakazi na jamii tunazozihudumia. Tunaingia katika hatua inayofuata kwa kujiamini kutokana na uongozi wetu, washirika wetu, watu wetu na mustakabali wa Tanzania,” alisema.
Meneja Mkaazi wa Watu Tanzania, Rumisho Shikonyi (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi, Watu, Bhavin Parmar (wa pili kushoto), Meneja Mkuu – Afrika Mashariki, Watu, Andrii Volokha (wa pili kulia) na Naibu Meneja wa Nchi, Watu Credit Tanzania, Seuri Kuoko (kulia), wakikata keki kama ishara ya kusherehekea kutimiza miaka mitano ya Watu Tanzania.
Mfumo wa utoaji huduma wa Watu Tanzania unaunganisha matumizi ya teknolojia na mtandao mpana wa mawakala wa ndani ili kufanya huduma za mikopo kuwa rahisi kufikiwa, kueleweka na kusimamiwa. Wateja wanaweza kufanya marejesho ya mikopo bila kutumia fedha taslimu kupitia huduma za fedha kwa njia ya simu pamoja na Programu ya Watu (Watu App), kulingana na ratiba za kila siku, wiki na mwezi.
Mbali na kutoa huduma za kifedha kwa wateja, Watu Tanzania pia imechangia katika kuongeza fursa za ajira na uongozi. Kwa sasa kampuni ina wafanyakazi zaidi ya 500 nchini kote, huku wanawake wakichangia takribani asilimia 43 ya nguvu kazi na kushika karibu nusu ya nafasi zote za uongozi.
Meneja Mkaazi wa Watu Tanzania, Rumisho Shikonyi, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Watu Tanzania, ambapo kampuni hiyo iliadhimisha miaka mitano tangu kuanza shughuli zake nchini Tanzania. Katika hotuba yake, alielezea safari ya Watu katika kupanua upatikanaji wa suluhisho za usafiri, mawasiliano na fursa za kifedha, huku akitambua mchango wa wateja, washirika, wadau na wafanyakazi waliochangia ukuaji wa kampuni hiyo chini ya kaulimbiu ya "Kila Mtu Ni Watu." Hafla hiyo ilifanyika tarehe 29 Juni 2026 jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, Watu Credit Tanzania ilitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mamlaka za udhibiti, mamlaka za Serikali za mitaa, taasisi za kifedha, wazalishaji, waendeshaji wa mitandao ya simu, wafanyabiashara, washirika wa teknolojia, wateja pamoja na wafanyakazi wake kwa mchango wao katika safari ya mafanikio ya kampuni kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Wakati Watu Credit Tanzania inapoanza hatua mpya ya ukuaji, kampuni inaendelea kujizatiti kupanua upatikanaji wa rasilimali za uzalishaji, kuwekeza katika teknolojia, kuimarisha ushirikiano na kuleta suluhisho inayowasaidia Watanzania.