Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaumma: Oktoba 29 hatutiki, tunapiga kura ya ukombozi

Mgombea ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya Chaumma, Moza Ally akihutubia wakazi wa Tandale Mbuyuni, katika kampeni jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 24, 2025. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo amesema Oktoba 29hawatiki bali wanakwenda kupiga kura ya ukombozi.

Akizungumza katika mkutano wa Kampeni wa kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni,  Moza Ally uliofanyika kata ya Tandale leo Septemba 24, 2025, Kileo amesema uchaguzi mkuu wa utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu si wa kutiki ni wa kwenda kupiga kura ya ukombozi.

Amesema siku hiyo ng'ombe atachinjwa alipoelekea, akiwasisitiza mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni kupiga kura ya ukombozi kwa Moza Ally.

"Tunapowaletea mtu kama Moza, tunawaletea kiongozi atakayekuwa sauti yenu, atakayesimama kwa niaba yenu, atakayekwenda bungeni kuondoa sheria kandamizi, huu ndio wakati wa Wanakinondoni na Watanzania kupiga kura ya ukombozi, hakuna kutiki," amesema Kileo.

Moza akizungumzia mikakati yake endapo atachakuliwa kuongoza jimbo hilo, ameanza kwa kuhoji ni vipi wananchi wa Tandale na Kinondoni wanakwenda kutiki wakati hawana maji kwenye nyumba zao.

Amesema huduma ya mama na mtoto hospitali wanailipia, watu wa Tandale wamechoshwa na mikopo kausha damu na kero nyingine, hivyo ni wakati sahihi kwa wao kutafakari vema na siku ya kupiga kura, wakaipige ya ukombozi kwa Chaumma.

"Nina mambo machache ya kuwaambia Wana Tandale na Kinondoni,  mkinipa ridhaa, kitu cha kwanza nitakachokwenda kukisimamia ipasavyo ni elimu.

"Mliambiwa elimu bure wakati mnachangishwa fedha, niazimeni imani, nikiwa mbunge hakutakuwa na mchango utakaoendelea wa kuwashulutisha wazazi mtoe elfu mbilimbili, nikiwa mbunge ili likitokea, mje kuripoti ofisi ya mbunge kwa hatua zaidi," amesema mgombea huyo.

Amesema atahakikisha shule zinakuwa na walimu wa kutosha na hakutakuwa na michango ya kuwalipa walimu wa ziada.

"Jambo jingine ni hedhi salama kwa mabinti zetu, nitakwenda kupambania bungeni ziondolewe kodi ili kila mzazi amudu kumnunulia mwanawe taulo za kike,” ameahidi Moza.

Akizungumzia suala la afya, Moza amesema; "Kwenye afya, kina mama tukienda hospitali kujifungua ni kama tunakwenda kununua watoto, huduma ya mama na mtoto Kinondoni mkinipa ridhaa itakuwa ni bure, tumeambiwa hivyo na mimi nitakwenda kulisimamia ili bungeni ili iwe bure kweli."

Amesema jambo lingine linalowaumiza wananchi ni la aliyeshiba kutomjua mwenye njaa. Moza amesema anawajua wenye njaa wenzake, akigusia adha ya watu kutakiwa kulipia gharama za matibabu za ndugu yao aliyepoteza maisha kuwa sehemu ya vitu atakavyohakikisha vinabaki kuwa historia Kinondoni.

"Vilevile tutafungua fursa za uchumi, tunahitaji kuwa na uchumi unaoeleweka," amesema Moza akigusia pia mkakati wa kuajiri mwanasheria kusaidia watu wote Kinondoni katika masuala ya kisheria bila kujali itikadi zao za vyama.

"Uwe ni CCM, Chaumma au chama kingine au usiye na chama naomba kura yako," amesema Moza.

Naye mgombea udiwani wa kata ya Tandale, Rahim Derenya ametumia nafasi hiyo kuomba kura akibainisha kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya kero ya maji katika kata hiyo.

Derenya amewaomba Watanzania Oktoba 29 kumchagua mgombea urais wa Chaumma, wagombea ubunge akiwamo Moza ambaye amesema anatosha kuwa mbunge wa jimbo, hilo kwa sababu ataleta maendeleo sambamba na kumpigia yeye kura ya udiwani wa kata hiyo.