Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CRDB Bank Foundation yatenga Sh400milioni kudhamini Imbeju Ndondo Cup

Dar es Salaam. Taasisi ya CRDB Bank Foundation imetenga jumla ya Sh400 milioni kudhamini mashindano ya msimu wa 13 wa Imbeju Ndondo Cup 2026.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa alisema kuwa  katika kiasi hicho, taasi zaidi ya shilingi milioni 100 zitatumika kama zawadi za timu bingwa, mshindi wa pili na zawad mbalimbal za wachezaji na mashabiki.

Tully alisema kuwa msimu huu unaleta fursa juu ya fursa kwa kila mdau wa Imbeju  Ndondo Cup.

Alisema kuwa bingwa wa mashindano haya atapata shilingi milioni 30 na mshindi wa pili atapata shilingi milioni 20.

Kwa mujibu wa Tully, katika kila hatua ambayo timu itafuzu itapata kiasi cha fedha ambacho kitangazwa baadaye.

Alisema kuwa mchezaji bora wa mashindano atazawadiwa sh3 milioni wakati mfungaji bora, beki bora na kipa bora atazawadiwa Sh1 milioni.

Kwa mujibu wa Tully, kutakiwa na zawadi ya Sh100,000 kwa kila mchezaji bora wa mechi na shabiki au kikundi cha bora kwa mechi katika ushangiliaji.

“Fedha hizi zitawekwa kwenye Akaunti ya Imbeju ya kila muhusika hivyo kutoa fursa juu ya fursa hali inayotimiza kaulimbiu ya Imbeju – Ndondo cup 2026 isemayo ‘Jiongeze,” alisema Tully.

Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekusudia  kufungua fursa kwa timu na wachezaji kutoka mtaani kuianza vyema safari yao ya kujijenga kiuchumi.

“CRDB Bank Foundation inathamini sana umahiri ndio maana imetoa kipaumbele kwa kila atakayeonyesha uwezo wa juu ndani ya uwanja na jukwaani walipo watazamaji kwa kumtambua mshabiki au kikundi cha mashabiki watakaonyesha upekee katika kushangilia,” alisema.

Alifafanua kuwa mbali ya mashindano na wachezaji kufurahia soka, vijana watapata elimu ya fedha na kufunguliwa Akaunti ya Imbeju kuwawezesha kusimamia mapato yao yatokanayo na vipaji vyao ili waweze kujenga uchumi imara, mafunzo ya uwekezaji na ujasiriamali pamoja na mafunzo ya ubunifu na fursa za uchumi wa kisasa.

Kwa upande wake, mratibu wa mashindano hayo, Yahaya Mohamed Mkazuzu alisema kuwa mpaka sasa mashindano hayo yameleta mafanikio kwa baadhi ya vijana kupitia mpira wa miguu.

Mkazuzu alisema kuwa wachezaji kama Idd Selemani Nado, Kelvin Sabato na Mashaka Pobga wamefanikiwa kupata nafasi ya kucheza timu kubwa kupitia mashindano hayo.

“Nawashukuru CRDB Foundation kupitia iMbeju kudhamini mashindano ya mwaka huu ambayo yanafikia msimu wa 13,” alisema Mkazuzu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mahusiano na Matukio wa Clouds Media Group, Shafii Dauda alisema kuwa iMbeju Ndondo Cup imefungua wigo pia kwa wafanyabiashara wadogo wadogo  mbali ya wachezaji.

Dauda alisema kuwa moja ya mkakati wao mkubwa ni kutumia iMbeju Ndondo Cup kuhamasisha mashindano ya Afcon  ya mwakani ambapo mbali ya Tanzania, pia mashindano hayo yanafanyika katika nchi za Kenya na Uganda.

“Naishukuru CRDB Foundation kwa kuwekeza nguvu katika mashindano haya ambayo yanatoa fursa kwa vijana na jamii pia,” alisema Dauda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mashindano wa Chama Cha soka cha mkoa wa Dar es Salaam, DRFA, Ramadhan Shauritanga aliahidi kusimamia mashindano hayo kwa uadilifu mkubwa na kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu