Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi atembelea Banda la GF katika Sabasaba

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la kampuni ya GF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), wakati wa hafla rasmi ya kufunga msimu wa maonesho ya mwaka 2026.

Katika ziara hiyo ya heshima, Rais Mwinyi alipokelewa na Mwenyekiti wa GF, Bw Mehboob Karmali, akiongozana na Mkurugenzi wa GF, Alijawad Karmali, pamoja na Mkurugenzi wa TANTRADE, Dk Latifa Mohammed.

Akiwa katika banda hilo, Rais Mwinyi alipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na GF pamoja na ubunifu wa kampuni hiyo katika sekta ya viwanda. Viongozi wa kampuni walieleza dhamira yao ya kuendelea kuzalisha bidhaa zenye viwango vya ubora wa kimataifa huku wakichangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia uwekezaji, ajira na maendeleo ya sekta ya viwanda.

Ziara ya Rais Mwinyi imeonekana kuwa ishara ya kutambua mchango wa sekta binafsi katika kuimarisha uchumi wa Taifa na kuendeleza azma ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda unaotegemea uzalishaji wa ndani. Kupitia maonesho hayo ya Sabasaba, GF imeendelea kuonesha nafasi yake kama miongoni mwa kampuni zinazochochea ubunifu na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotengenezwa nchini.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, uongozi wa GF ulieleza kuwa umetunukiwa heshima kubwa kwa kutembelewa na Rais wa Zanzibar, ukisema ziara hiyo ni chachu ya kuendelea kuwekeza katika ubora, teknolojia na uzalishaji unaokidhi mahitaji ya Watanzania.

Kampuni hiyo pia imeishukuru TANTRADE kwa maandalizi ya mafanikio ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, huku ikitoa shukrani kwa wateja, washirika wa biashara na wananchi wote waliotembelea banda lake katika kipindi chote cha maonesho.

Ikiendelea kusimamia kaulimbiu ya "Built in Tanzania for Tanzanians", GF imesisitiza kuwa itaendelea kuwa mshirika muhimu katika safari ya Tanzania kuelekea maendeleo ya viwanda na uchumi imara, ikiongozwa na falsafa yake ya "Moving Together" ya kushirikiana kujenga taifa lenye ustawi na maendeleo endelevu.