Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Grace Kiwelu arejesha fomu ya ubunge Vunjo, wasisitiza haki uchaguzi mkuu

Mtiania wa nafasi ya ubunge Jimbo la Vunjo kupitia chama cha ukombozi wa umma (Chaumma), Grace Kiwelu akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo hilo Msimamizi wa uchaguzi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema mara baada ya kurejesha fomu hiyo leo, Agosti 14, 2025.

Muktasari:

  • Lema ameyasema hayo leo Agosti 14, 2025 wakati wa shughuli ya urejeshaji wa fomu iliyoenda sambamba na uzinduzi wa ofisi ya chama hicho zilizopo eneo la Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Moshi. Mtiania nafasi ya ubunge kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Grace Kiwelu amerejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Vunjo, huku katibu wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema akitaka uchaguzi uwe wa huru na haki.

Lema ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 14, 2025 wakati wa shughuli ya urejeshaji wa fomu iliyoenda sambamba na uzinduzi wa ofisi ya chama hicho zilizopo eneo la Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

"Mimi ninachotaka ni uchaguzi wa haki tuu, huku ndani ya chama tugombee kwa haki na huko nje tuletewe wanayemleta tuingie kwenye uchaguzi wa haki, mwaka huu tumejipanga vizuri, tutakutana kwenye sanduku la kura, tutashughulika mwaka huu haiwajawi kutokea," amesema Lema. 

Amesema "Tunawaambia watu wa Vunjo pamoja na mbinu zetu nyingine nyingi mtu akipiga kura ailinde kura yake, kule ndani tutaweka mawakala, barabarani tutaweka mawakala, nje ya kituo cha kupigia kura tutaweka watu na kama kuna mtu ana mpango wa kituibia kura asahau."

Pamoja na mambo mengine, ameonya vitendo vya rushwa katika uchaguzi na kusema chama hicho kipo tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Aidha, amesema chama hicho kinaendelea kupokea fomu za ubunge na udiwani mpaka Agosti 26, mwaka huu na tayari watiania wa ubunge katika majimbo Sita ya Mkoa huo wameshachukua fomu.

"Tutaendelea kupokea fomu mpaka Agosti 26, mwaka huu, hivyo yoyote anaweza kuwa na nia ya kugombea ubunge au udiwani kupitia chama cha Chaumma katika Jimbo aliko, hivyo hatufungi milango, sisi tupo huru," amesema Lema.

Kiwelu amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumsindikiza kuchukua fomu na kwamba imani yake kwao ni kubwa na hawatamuangusha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

"Niwashukuruni sana kwa kunisindikiza ndugu zangu, ninaujua upendo wenu nimeuona tangu 2020 niwashukuru sana kwasababu mlinipa kura za kutosha, lakini nashukuru kwa yaliyotokea,"amesema Kiwelu.

Mtiania wa ubunge Jimbo la Same Magharibi, Gervas Mgonja ambaye alichukua fomu jana, aliwashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumuunga mkono kuhakikisha anagombea katika Jimbo hilo.

"Ndugu zangu nimeamua kugombea nafasi hii si kwa sababu ya kutafuta heshima binafsi bali kwa mapenzi makubwa niliyonayo kwa watu wa Same Magharibi," amesema Mgonja.