Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jengo la vifaa vya kilimo lazinduliwa Kilolo, Wakulima wahimizwa kilimo tija

Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Estomin Kyando, Mwenyekiti wa bodi ya Farm For The Future (FFF), Osmund Ueland na viongozi wengine wa FFF wakizindua jengo la kuhifadhia zana za kilimo lililopo FFF Ilula wilayani Kilolo.Picha na Christina Thobias

Muktasari:

  • Jengo la vifaa vya kilimo lazinduliwa Kilolo likiwa na mashine za kisasa, matrekta na zana nyingine huku serikali ikiimiza kutumia teknolojia na pembejeo za ruzuku kuongeza tija katika kilimo.

Iringa. Katika mchakato wa kuongeza tija kwa wakulima na kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kilimo, Serikali kwa kushirikiana na wawekezaji mkoani Iringa imezindua jengo la kisasa la vifaa vya kilimo katika Wilaya ya Kilolo, lenye mashine za kuvuna, kupanda na kuhifadhi mazao, hatua inayolenga kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza mavuno kwa wakulima.

‎Jengo hilo lenye vyumba vitatu linahifadhi zana mbalimbali zikiwemo mashine ya kuondoa mawe kabla ya upandaji wa viazi, mashine ya kupandia viazi na matrekta mapya yatakayowasaidia wakulima kuongeza ufanisi wa kazi zao.

‎Akizindua jengo hilo Leo Disemba 7, 2025 katika kampuni ya Farm For the Future iliyopo Ilula mkoani Iringa, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Estomin Kyando amesema Serikali kwa kushirikiana na wawekezaji imejipanga kuwapiga jeki wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku pamoja na kuimarisha miundombinu ya kilimo ikiwemo upatikanaji wa zana.

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo akizungumza na Wakukima juu ya umuhimu wa kutumia teknolojia kwenye kilimo katika hafla ya uzinduzi wa jengo la zana za kilimo katika eneo la kampuni ya Farm For the Future Ilula mkoani Iringa.Picha na Christina Thobias

‎DC Kyando amesisitiza kuwa mafunzo yanayotolewa kwa wakulima hayapaswi kubaki kwenye nadharia bali yahitaji kufanywa kwa vitendo ili kuongeza tija.

‎“Ukibebwa bebeka, fursa ndio hizi hivyo Wakulima mnapaswa kuchangamkia teknolojia hizi ili muondokane na kilimo cha mazoea,” amesema DC Kyando.

‎Mwenyekiti wa bodi ya Farm For The Future (FFF), Osmund Ueland amesema uzinduzi wa jengo jipya la vifaa vya kilimo wilayani Kilolo utawapatia wakulima fursa ya kupata zana bora na huduma za ugani kwa urahisi, hali itakayochochea kilimo cha tija katika eneo hilo.

‎Osmund amesema jengo hilo ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuhakikisha wakulima wanapunguza gharama za uzalishaji na kuongezeka kwa mavuno kupitia teknolojia ya kisasa.

‎Akizungumza na Mwananchi Digital, Osmund amesema FFF imekuwa ikipokea maoni ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali na kuyatumia kuboresha huduma wanazotoa, ikiwemo ushauri wa kitaalamu, upatikanaji wa mashine na mbegu bora.

Wakulima kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Kilolo wakiwa eneo la Farm For the Future wakisikiliza ushauri wa matumizi ya zana za teknolojia ya kilimo katika shughuli za kilimo.Picha na Christina Thobias

‎"Ushirikiano na kampuni zinazouza zana za kilimo na pembejeo utaendelezwa ili wakulima wasikose huduma muhimu wakati wa msimu," amesema Osmund

‎Katika hatua nyingine Osmund amesema pamoja na kutoa huduma za kilimo, taasisi hiyo imejipanga kuimarisha miundombinu muhimu inayohitajika kuendeleza kilimo, ikiwemo barabara za kupitisha mazao na visima vya maji kwa ajili ya shughuli za shambani.

‎Osmund ameongeza kuwa miundombinu hiyo ni muhimu katika kuinua uzalishaji na kupunguza changamoto ambazo zimekuwa zikiwakwamisha wakulima wengi vijijini.

‎Aidha Osmund amesisitiza kuwa lengo la mradi huo ni kuimarisha uchumi wa mkulima kwa kumpa uwezo wa kufanya kilimo chenye tija na matumizi ya teknolojia rahisi na nafuu.

‎Pia Osmund amewataka wakulima kuendelea kushiriki mafunzo na kutoa maoni ili huduma zinazotolewa ziweze kumfaa mkulima moja kwa moja.

Jengo la vifaa vya kilimo lililozinduliwa Ilula katika Kampuni ya Farm For the Future Kilolo likiwa na mashine za kisasa, matrekta na zana nyingine za teknolojia ya kilimo. Picha na Christina Thobias

‎“Kila pendekezo la mkulima ni sehemu ya mipango yetu ya utekelezaji, tunataka huduma zinazotolewa ziwe suluhisho la changamoto zao halisi kwenye kilimo,”Amesema Osmund

‎Maafisa kilimo kutoka halmashauri tofautitofauti mkoani iringa wamesema kwamba vifaa hivyo vitarahisisha kazi mashambani na kuongeza uzalishaji wa mazao hususani viazi.

‎Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Underhaug Norway inayotengeneza vifaa vya teknolojia za kilimo, Arild Hoien ameiambia Mwananchi Digital kuwa kampuni hiyo itaendeleza uwekezaji wake hadi mwaka 2026 sambamba na kuimarisha ushirikiano na Farm For The Future.

‎Kwa upande wao Wakulima kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Kilolo wamesema kwamba FFF wamekuwa msaada kwao kwa uwepo wa miradi tofautitofauti ya kilimo na kupitia jengo hilo kutawezesha Wakulima kupata pembejeo eneo jirani zaidi

Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Okoa kilichopo Image 8 Wilayani Kilolo, Petro Mwinuka amesema wanatarajia kutoa elimu kwa wakulima 150 juu ya matumizi ya zana za kisasa kwa mikopo nafuu, huku Norbert Longo wa AMCOS ya Vitono akisema teknolojia hizo zitawanufaisha wakulima wa eneo hilo.

‎Kwa upande wa Kampuni ya YARA, Mwakilishi wa kampuni hiyo, Laurent Shija amesema kupitia kituo hicho, wakulima watanunua mbegu bora na mbolea zilizothibitishwa, hatua iliyosaidia kuongeza uzalishaji kwa wakulima wa Kilolo.