Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia zawanufaisha washindi 80 kupitia kampeni ya Mixx

Dar es Salaam. Wakati kombe la dunia likifikia tamati Julai18,2026, Watanzania wameendelea  kunufaika nje ya uwanja kupitia kampeni ya  ya Kombe la Duniaya "Kila Muamala ni Bao la Ushindi" ambapo washindi 80 wamejishindia fedha taslimu na vifaa vya kisasa vya Hisense.

Kampeni hiyo, inayohusisha matumizi ya Mixx Super App kufanya malipo ya huduma mbalimbali za kifedha, imeendelea kuongeza msisimko kwa wateja, huku zawadi zikiendelea kutolewa kila wiki.

Katika droo ya wiki ya nane iliyofanyika Dar es Salaam, washindi sita walitangazwa. Wanne walikabidhiwa fedha taslimu za Sh1 milioni kila mmoja, huku wawili wakiondoka na vifaa vya kisasa vya Hisense.

Baadhi ya washindi hao ni  washindi Dadi Likuta, Elias Sagiro, John Mkonyi na Ibrahim Mandoa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Malipo ya Kidijitali wa Mixx, Mshamma Mshamma, alisema mwitikio wa wateja wao umekuwa mkubwa tangu kampeni ilipoanza.

Mchamma Alisema hadi sasa washindi 80 tayari wamejinyakulia zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu na vifaa vya Hisense, kupitia ushirikiano wa Mixx na kampuni hiyo ya kutengeneza vifaa vya elektroniki.

"Kampeni hii inazidi kushika kasi na baada ya wiki mbili, tutafanya droo kubwa ambapo mshindi atazawadiwa Sh50 milioni. Tumekuwa tukitoa zawadi kwa siku ambapo washindi wanapata Sh1 milioni na vifaa vya elektroniki kutoka Hisense. Huu ni uwekezaji mkubwa kwa wateja wetu na tunaomba waendelee kushiriki,” alisema Mchamma.

Alisema kuwa lengo la kampeni hii hasa kwa kutumia Mixx Super App. ni kurahisisha huduma za kifedha na wakati huo huo kuwazawadia watumiaji.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo bado haijafikia tamati, huku zawadi kubwa ya Sh50 milioni ikisubiri mshindi wa mwisho, jambo ambalo linaendelea kuongeza ushindani miongoni mwa watumiaji wa programu hiyo.

Aliwahamasisha Watanzania kuendelea kufanya malipo ya huduma mbalimbali kupitia Mixx Super App ili kuongeza nafasi ya kushiriki droo na kujishindia zawadi.

Kwa upande wake, mmoja wa washindi, Ibrahim Mandoa wa Kinondoni, alisema ushindi wake umethibitisha kuwa kampeni hiyo ni ya kweli na imekuwa ikiwanufaisha watumiaji wa kawaida.

"Sikutegemea kushinda, lakini leo nimejionea mwenyewe. Ninawahimiza Watanzania kutumia Mixx Super App kufanya malipo yao kwa sababu nafasi ya kushinda ipo kwa kila mtumiaji," alisema.

Kupitia kampeni hiyo, Mixx imeongeza msisimko wa Kombe la Dunia na matumizi ya huduma za kifedha kidijitali, huku mamia ya watumiaji wakiendelea kusubiri droo zinazofuata kwa matumaini ya kuingia kwenye orodha ya washindi, ikiwemo mshindi atakayenyakua kitita cha Sh50 milioni mwishoni mwa kampeni.