Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masauni aelekeza NCMC kutoa elimu ya biashara ya kaboni kwa wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Azimio iliyopo Halmashauri ya Mji Rufiji mkoani Pwani (hawapo pichani) alipokuwa mkoani humo kwenye ziara yaa kikazi, Julai 21, 2026.

Pwani. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamadi Yussuf Massauni amekielekeza Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) mkoani Morogoro kutoa elimu ya Biashara ya Kaboni kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Masauni ameyasema hayo wakati akiwa wilayani humo kwenye ziaraa ya kikazi, Julai 21, 2026 wakati akieleza fursa na faida za uhifadhi wa mazingira ukiwemo utunzaji wa misitu.

Amesema wakazi wa Rufiji wanapaswa kutumia fursa katika biasharara ya kaboni kujikwamua kiuchumi na Ofisi ya Makamu wa ipo tayari kutuma wataalam kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi waliokuwa tayari kufanya biashara hiyo.

"Sina uhakika kama mmeshaanza ila kama bado mnaweza kuanza ili mfike mbali zaidi, miradi ya utunzaji wa Mazingira ikiwemo migomba, mikorosho ni biashara nzuri kwenye kaboni, watumieni wataalamu wawape muongozo kuongeza kipato ili kutumia fursa hii," amesema Waziri Masauni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Tarura Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mhandisi Nicolaus Ludigery (katikati) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami wilayani humo, Julai 21,2026.

Waziri Masauni pia amesema mabadikiko tabia nchi ni chanzo cha biashara hiyo ndio na kwamba kupitia mkataba wa Paris walikubaliana nchi zenye rasilimiali katika kupunguza hewa ya ukawa zilipwe.

"Utakuta misitu imezagaa zagaa watu wanakata miti ovyo bila kukua hii ni biashara inaweza kuwakwamua kiuchumi hata mtu mmoja mmoja au vikundi", amesema.

"Lengo letu tunataka kila fursa inayogusa fursa kwenye biashara ya kaboni inafumika ipasavyo wanarufiji, mkitumia fursa hii vizuri itawasaidi wengi wenu kwani walioanza tayari wanavuna matunda,”," Amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema mkoa huo kwasasa unaongoza katika mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, ujenzi wa viwanda na ufaulu katika sekta ya elimu.

Kunenge amesema uwekezaji mkubwa umefanyika ikiwemo kiwanda cha sukari ambacho kimejengwa Rufiji na Viwanda vingine ambavyo vinakuza ajira kwa mji huo.

Amesema muelekeo wa Serikali kuelekea katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050 ni kuwa na ajira zaidi na kuongeza mapato ya nchi ambapo kila mmoja itamgusa katika eneo lake.