Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwongozo kwa wanahabari na watengeneza maudhui jamii za pembezoni waandaliwa

Muktasari:

  • Mwongozo huo, unatarajiwa kuwasaidia Wanahabari na Watengeneza maudhui, kutambua maadili na miiko ya jamii za pembezoni za Wahadzabe, Masai, Datoga na Akie, kabla ya kuandika na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Arusha. Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni(UNESCO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni(MAIPAC) na Idara ya Habari Maelezo, wameanza mpango wa kutengeneza mwongozo mpya kwa ajili ya watengeneza maudhui katika maeneo ya jamii za pembezoni.

Mwongozo huo, unatarajiwa kuwasaidia Wanahabari na Watengeneza maudhui, kutambua maadili na miiko ya jamii za pembezoni za Wahadzabe, Masai, Datoga na Akie, kabla ya kuandika na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo duniani (WPFD) jijini Arusha,Mkurugenzi wa mtendaji wa Taasisi ya MAIPAC, Mussa Juma amesema mwongozo utahusiana na waandaji wa maudhui mitandaoni na matumizi ya akili Unde katika kuboresha kazi zao.

Juma amesema katika katika siku za karibuni wameibuka watengeneza maudhui wa ndani na nje ya nchi, Kwenda moja kwa moja katika maeneo ya jamii hizo hasa Wahadzabe na kutoa maudhui yao bila ridhaa yao na maudhui mengine ambayo ni kinyume cha maadili.

“Kutokana na changamoto hii, MAIPAC kwa kushirikiana na UNESCO na Idara ya Habari Maelezo tumeanza utekelezaji wa uandaaji wa mwongozo maalum wa kufanyakazi katika jamii hizi kwa kuzingatia maadili na bila kudhalilisha utu wa jamii hizi".

Amesema sambamba na mradi huo, pia MAIPAC kwa kushirikiana na UNESCO, Maelezo na SAVVY Media, wanatarajia kusaidia jamii hizi kujua matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii lakini pia kuanza kunufaika na matangazo na Habari ambazo zimekuwa zikitangazwa kuwatumia wao.

“Tutazijengea uwezo jamii hizi, kuweza kutumia vizuri mitandao kwa manufaa yao pia kiuchumi na kutambua haki zao mbali mbali za kidigitali na hivyo kuinua Uchumi wao”alisema

Wakizungumza katika mjadala huo, baadhi ya watengeneza Maudhui mitandaoni na Maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), walisema matumizi ya mitandao na akili unde vinapaswa kusaidia vijana na jamii badala ya kuopogwa.

Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe katika eneo la bonde la Eyasi, wilaya ya Karatu, Mdindi Samboga alishukuru MAIPAC,UNESCO,Maelezo na SAVVY Media, kuja na mradi wa kuwasaidia.

Samboga alisema jamii yao imepata umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii katika siku za karibuni lakini hata hivyo hainufaiki na wanaotengeneza picha na Habari.

“Wanakuja wanatupiga picha na kutuhoji tunasikia mijini tunaonekana sana lakini sisi hatunufaiki zaidi ya kupewa pombe, sasa tunaomba kusaidiwa kunufaika na utamaduni wetu”amesema