Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NRA yaahidi kudhibiti mabando ya simu, kugawa mashine za EFD bure

Muktasari:

Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimeahidi kushughulikia utaratibu wa mitandao ya simu kuweka ukomo wa matumizi ya vifurushi na inapofikia muda husika bila kutumika kifurushi kinachukuliwa na mtandao wa simu, ikieleza ni mfumo wa wizi uliohalalishwa.

Kigoma. Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimezindua kampeni kikitaja maeneo 23 ya kipaumbele katika ilani yake ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kikiwa na kaulimbiu isemayo: “Taifa kwanza vyama baadaye.”

Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo Septemba 5, 2025 katika Kata ya Buzebazeba, Jimbo la Kigoma Mjini, mgombea urais wa chama hicho, Almas Hassan amesema akipata ridhaa ya wananchi ya kuongoza Serikali atadhibiti wizi wa kimtandao.

Amesema wizi huo unatokana na mifumo ya mitandao ya simu kuwa na vifurushi vyenye ukomo wa muda hali inayowafanya wamiliki wa mitandao kuwa matajiri kuliko watumiaji wa vifurushi.

Amesema utaratibu wa mitandao ya simu kuweka ukomo wa matumizi ya vifurushi na inapofikia muda husika bila kutumika kifurushi kinachukuliwa na mtandao wa simu ni mfumo wa wizi uliohalalishwa, unaowanyonya wananchi, huku wamiliki wa mitandao wakiendelea kunufaika.

“Mlishawahi kuona mtu ananunua mchele halafu kesho muuza duka anakuja asubuhi anasema nimeijia mchele wangu, kila mtu anaibiwa siyo walinzi, majaji hata wazee wangu kule ziwani? Kwa nini hawajifunzi kwa Tanesco ambao hawana kikomo?’’ amehoji.

Hassan amesema: “Nikiwa Rais ndani ya siku 30 nitawaita watu wa mitandao waje waseme bando zetu wanapeleka wapi na watalipa, huu umekuwa wizi usio na kesi wala mashtaka na mwisho wake 2025.’’

Amesema endapo atashinda kiti cha urais, atapiga marufuku mapenzi ya jinsia moja akieleza vyama vingine vinayaonea haya kuyasema.

Mgombea huyo amesema ikiwa Serikali haiwezi kukemea tabia hizo, katika kipindi cha miaka 40 ijayo hakutakuwa na wanaume au wanawake wenye nguvu ya kufanya kazi.

Ili kuwa na jamii iliyostawi amesema afya litakuwa jambo la kipaumbele, akiahidi matibabu yatatolewa bure kwa kila mwananchi isipokuwa matibabu ya anasa akitoa mfano wa kubadili uso na kuongeza shepu.

Ameahidi kupunguza idadi ya wizara serikalini na kuwa 10, akisema uwepo wa nyingi unaongeza mzigo wa utendaji, huku mawaziri wengi wakiwa wasio na taaluma ya wizara wanazoziongoza.

Katika ukusanyaji wa kodi, NRA imeahidi kugawa mashine za kielekroniki za kutolea risiti (EFD) bure kwa wafanyabiashara na zitatungwa sheria kali kuwalazimisha wafanyabiashara kutoa risiti.