Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya Rama Ngozi kupambana na uhalifu mtandaoni

New Content Item (4)
New Content Item (4)

Muktasari:

  • Rama Ngozi bado anaendelea kuwa mfano wa wataalamu wanaochangia kulinda maisha ya kidijitali ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa usalama mtandaoni ni jukumu la kila mtumiaji.

Dar es Salaam. Katika zama za sasa ambazo matumizi ya mitandao ya kidijitali yanazidi kukuwa kwa kasi, mtaalamu wa teknolojia ya habari, Ramadhani Ngozi maarufu kama Rama Ngozi, ameibuka kuwa miongoni mwa vinara wa kupambana na uhalifu wa mitandaoni nchini.

Akiwa na shauku kubwa ya teknolojia, Ngozi amejikita katika kusaidia watumiaji wa mitandao ya kijamii kulinda akaunti zao dhidi ya wizi wa akaunti za watumiaji na kuwadhibiti matapeli wanaotumia majina bandia.

Akizungumza kuhusu kazi yake, Ngozi anasema lengo lake ni kuhakikisha watumiaji wanakuwa salama mtandaoni kwa kuthibitisha akaunti zao na kuwapa elimu ya kujikinga na wadukuzi.

“Ni muhimu kwa watumiaji kutambua hatari zilizopo na kuchukua hatua za kujilinda,” anasema Ngozi.

Mbali na uhakiki wa akaunti, mtaalamu huyo hutoa elimu kwa jamii kupitia semina na warsha mbalimbali, akielekeza namna ya kutambua ujumbe wa kitapeli (phishing), kuweka nywila imara na kulinda taarifa binafsi.

Taarifa zinaeleza kuwa kuongezeka kwa akaunti feki na matukio ya kujifanya watu wengine mtandaoni kumeifanya kazi ya Ngozi kuwa muhimu zaidi katika kuhakikisha uhalisia wa mawasiliano ya kidijitali.

Aidha, Ngozi ameshirikiana na kampuni mbalimbali zinazo tumia mitandao ya kijamii ili kuboresha mifumo ya usalama wao, hatua inayochangia kupunguza mianya ya uhalifu mtandaoni.

Kwa mujibu wa wataalamu, juhudi kama hizi zinahitajika zaidi wakati huu ambapo matumizi ya mtandao yanaongezeka huku hatari za wadukuzi nazo zikiendelea kushamiri.

Kwa ujumla, Rama Ngozi anaendelea kuwa mfano wa wataalamu wanaochangia kulinda maisha ya kidijitali ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa usalama mtandaoni ni jukumu la kila mtumiaji.