Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatoa Sh22 milioni kuhamasisha matumizi ya nishati safi Shuleni

Tanki la gesi la nishati safi ya kupikia yenye thamani ya Sh22 milioni kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari Liwale.

Muktasari:

  • Serikali yatoa Sh22 milioni kwaajili ya majiko ya kisasa ya kupikia ili kuepukana na matumizi ya nishati chafu.

Liwale. Serikali imetoa majiko pamoja na tanki la gesi la nishati ya kupikia yenye thamani ya Sh22 milioni kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari Liwale ili kuondokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.

Msaada huo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama, hususan katika taasisi za umma kama shule, ili kulinda afya za watumiaji pamoja na mazingira.

Hatua hiyo pia inalenga kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ambao huchangia uharibifu wa misitu na ongezeko la hewa ukaa.

Mmoja wa wapishi wa Shule ya Sekondari Liwale akizungumza leo Jumanne Aprili 28,2026 mara baada ya kuzindua matumizi ya nishati safi  na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda ,Amina Mohamed ameishukuru Serikali kwa jitihada za kutenga fedha na kuwapatia majiko hayo, akisema kuwa yatarahisisha kwa kiasi kikubwa shughuli za upishi shuleni hapo.

Maimuna Saidi akipika chakula cha wanafunzi kwa kutumia nishati safi ya kupikia

Amesema kuwa awali walikuwa wanatumia kuni na mkaa na walikuwa wanapata changamoto kubwa katika kupika chakula kwa idadi kubwa ya wanafunzi, hali iliyosababisha ucheleweshaji wa chakula na wakati mwingine kuathiri ratiba za masomo.

“Tunai­shukuru Serikali kwa juhudi kubwa waliyoifanya ya kutupatia vifaa hivi kwani vinatusaidia sana kupika kwa haraka na watoto wanapata chakula kwa wakati. Mwanzoni tulikuwa tunachelewa kumaliza kupika, lakini sasa hivi tunapika ndani ya saa moja tu,” amesema.Mohamed

Aidha, ameongeza kuwa matumizi ya gesi yanapunguza moshi jikoni hali inayosaidia kulinda afya za wapishi na kupunguza madhara ya magonjwa ya mfumo wa upumuaji yaliyokuwa yakisababishwa na moshi wa kuni na mkaa.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Emanuel Nakey, naye ameishukuru Serikali kwa juhudi hizo akibainisha kuwa majiko hayo ya kisasa yameleta mabadiliko chanya katika uendeshaji wa shughuli za shule.

“Tunaishukuru Serikali kwa jitihada kubwa walizozifanya. Majiko haya yatatusaidia sana katika kuokoa muda, kuboresha mazingira ya upishi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi,” amesema Nakey.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu pia katika kulinda mazingira kwani matumizi ya nishati safi hupunguza ukataji wa miti hovyo na hivyo kusaidia kuhifadhi rasilimali za misitu kwa vizazi vijavyo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameeleza kufurahishwa na mabadiliko hayo wakisema kuwa sasa wata,pata chakula kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, hali inayowawezesha kuzingatia zaidi masomo yao.

Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa taasisi mbalimbali kuhamia katika matumizi ya nishati safi ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, hususan katika sekta ya elimu, afya na hifadhi ya mazingira.

Hata hivyo mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda wamewapongeza kwa juhudi kubwa waliyoifanya ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu lakini pia amewataka watu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji kutoa elimu kwenye taasisi zote zinazotoa huduma ya nishati safi ili kuweza kujikinga na majnga ya  moto.