Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaweka mkazo sanaa, michezo kuwa ajira kwa vijana

Dar es Salaam. Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha sekta ya sanaa na michezo inakuwa miongoni mwa maeneo yanayotoa ajira na kuchochea maendeleo kwa vijana nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Tarafa wa Lisekese, Emmanuel Shilatu, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya Masasi katika uzinduzi wa mashindano ya Kanda ya Kusini ya kusaka vipaji vya sanaa na michezo kwa watoto, yanayoandaliwa na Shirika la Compassion International.

Shilatu amesema Serikali imeweka kipaumbele katika kuendeleza vipaji vya wanafunzi na vijana kwa kuimarisha ushirikiano na wadau wa michezo na sanaa.

“Serikali imeweka vipaumbele vyake katika kuendeleza vipawa na vipaji vya wanafunzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo. Hivi karibuni Serikali imeboresha mfumo wa elimu kwa ajili ya kuwaandaa vijana kujifunza amali mbalimbali zikiwemo za michezo na vipaji vya sanaa,” amesema.

Amesema hatua hiyo inalenga kuwapa vijana fursa ya kutumia vipaji vyao kama nyenzo ya kujiajiri na kujenga maisha yao ya baadaye.

Kwa upande wake, mwandaaji wa mashindano hayo kutoka Compassion International amesema jukwaa hilo linatoa nafasi kwa watoto na vijana kuonyesha uwezo wao, kujenga nidhamu na kuandaa msingi wa mafanikio katika safari zao za vipaji.

Amesema mashindano hayo yanalenga kuhakikisha washiriki wanapata mazingira bora yenye ushindani wa haki, ubora na burudani.

Mmoja wa wazazi, Prisca Richard, ambaye mtoto wake anashiriki mashindano hayo, amesema amepongeza mpango huo akisema unasaidia kukuza vipaji vya watoto na kuwapa matumaini ya kufikia ndoto zao.

Mashindano hayo yanashirikisha watoto na timu kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.

Yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 26, 2026 ambapo mgeni wa heshima katika hafla ya kufunga anatarajiwa kuwa Waziri wa Vijana, Joel Nnauka.