Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wacheza gofu 150 kushiriki Vodacom Corporate Masters

Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc Joseph Sayi (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Vodacom Corporate Masters yaliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Lugalp Agosti Mosi. Kushoto ni mwenyekiti Corporate Masters, Ken Kariuki Mbaya na kulia ni katibu wa mashindano hayo, Maryanne Mugo.

Dar es Salaam. Jumla ya wachezaji wa Gofu 150 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya Vodacom Corporate Masters yaliyopangwa kufanyika Agosti Mosi kwenye uwanja wa gofu wa Lugalo. 

Mbali ya Vodacom Tanzania limited washirika wengine  wa mashindano hayo yaliyozinduliwa jana, washirika wengine wa mashindano hayo ni Oakwood Holdings Limited.

Wachezaji hao wanaume, wanawake na chipukizi wanatoka klabu mbalimbali nchini na baadhi ya nchi jirani, mashindano hayo yatakuwa ya mashimo 18 kwa mtindo wa stroke play. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc Joseph Sayi alisema mashindano hayo yanadhihirisha dhamira ya Vodacom ya kuimarisha uhusiano wake na jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania na ndio maana wameamua kudhamini kwa mwaka wa tatu mfululizo. 

"Vodacom tunaamini kuwa ukuaji endelevu wa biashara unajengwa kupitia mahusiano imara na yenye maana. Mashindano ya golf ya Vodacom Corporate Masters 2026 ni zaidi ya mashindano ya michezo, hili ni jukwaa linalowakutanisha viongozi wa biashara, wabunifu na watoa maamuzi ili kujenga uhusiano, kubadilishana mawazo na kusaka fursa mpya zitakazochangia ajenda ya Tanzania ya mageuzi ya kidijitali.

 Kupitia mpango huu tunaendelea kuziwezesha biashara kwa kutoa suluhisho za teknolojia zenye uhakika huku tukiwapa wateja na wadau wetu uzoefu wa kipekee," alisema Sayi.

Katika kipindi chote cha mashindano hayo, Vodacom Business itaonesha suluhisho zake bunifu za kidijitali zinazojumuisha huduma za mawasiliano, usalama wa kidijitali pamoja na teknolojia za biashara zinazosaidia taasisi kuongeza ufanisi wa shughuli zake, kuharakisha ukuaji na kuendelea kuwa na ushindani katika dunia inayozidi kutegemea teknolojia. 

Washiriki pia watapata fursa ya kukutana na viongozi wa Vodacom na kupata uelewa wa suluhisho mbalimbali zinazokidhi mahitaji yanayobadilika ya biashara.

Mwenyekiti wa Corporate Masters, Ken Kariuki alielezea mashindano hayo kuwa ni jukwaa la kipekee la ushirikishwaji wa makampuni linalowezesha kuongeza muonekano wa chapa, kujenga mitandao ya kibiashara, kuzalisha fursa za biashara na kuimarisha ushiriki wa wateja.

Tukio hilo la siku moja litashirikisha timu 10 za makampuni zitakazoshindania kombe la Vodacom Corporate Masters 2026, sambamba na eneo maalum la makampuni litaklokuwa na burudani, maonesho mbalimbali, maonesho ya vitu vya kale (vintage) pamoja na eneo maalum la watoto, hivyo kuweka mazingira rafiki kwa familia, kwa washiriki na wageni watakaohudhuria.

Mashindano ya golf ya Vodacom Corporate Masters yanaendelea kudhihirisha dhamira ya Vodacom Tanzania ya kujenga ushirikiano wa kuaminika na kuunga mkono mipango inayozalisha thamani ya kudumu kwa wateja, biashara na jamii. Kwa kuunganisha michezo, biashara na ubunifu, Vodacom inaendelea kuimarisha nafasi yake kama mshirika wa kuaminika katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali.