Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wavishukia viwanda vinavyotitirisha maji yenye kemikali

Wadau wa mazingira nchini Pakistan wamedai viwanda vinatiririsha maji yenye kemikali katika baadhi ya mito jambo linalohatarisha afya za wananchi.

Huku wakitaja maeneo yaliyoathirika zaidi ya Lahore, Sindh na Ziwa Manchhar linalotumika kwa shughuli za uvuvi na umwagiliaji, wamesema serikali inatakuwa kuchukua hatua za haraka kwani kuna baadhi ya maeneo kuna magonjwa ya mlipuko.

Hivi karibuni mamlaka inayosimamia mto Indus ilikosoa namna viwanda vinavyotumia maji ya Ziwa Manchhar, zikieleza kuwa yanatumika ndivyo sivyo.

‘’Mto Ravi huko Punjab umekuwa mojawapo ya mifano, awali ulikuwa kitovu cha ikolojia na kilimo mjini Lahore na katika wilaya zinazozunguka lakini kwa sasa mto huo unapokea kiasi kikubwa cha maji taka,’’

‘’Katika sehemu nyingi uchafuzi wa maji umekuwa mkubwa na wananchi wanaripoti maji kutoa harufu kali. Uchafuzi wa viwanda na usimamizi duni wa maji imeharibu ubora wa maji katika maziwa na kuwaathiri wavuvi na wakulima,’’ alisema Dk Medrick Khan.

Wadau hao wa mazingira wamebainisha kuwa eneo la Khyber Pakhtunkhwa uharibifu unaoongezeka hasa katika mito ya Kabul na Swat na kusababisha magonjwa ya mlipuko.

Mapema mwaka huu Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto (Unisef) lilitoa ripoti inayoonesha baadhi ya wananchi Pakistan kutumia maji ambayo si salama.

Khan alidai katika maeneo kadhaa ya mijini maji machafu ya mito huingia kwenye vyanzo vya maji vya chini ya ardhi na hivyo kuzidisha wasiwasi wa usalama wa maji.

Walisema licha ya nchi hiyo kuwa na sheria na kanuni za kudhibiti matumizi yasiyofaa ya maji, utekelezaji wake unasuasua na wahusika hawachukuliwi hatua stahiki.