Wanadiplomasia waishauri Pakistan kuhusu mgogoro wa Iran
Ukaribu wa Pakistan na Saudi Arabia umewaibua wanadiplomasia na kulishauri Taifa hilo kutoisaidia kijeshi Saudi Arabia kwa madai kuwa itajiingiza moja kwa moja katika mgogoro kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Saudi Arabia ni kati ya mataifa yenye kambi za kijeshi za Marekani na baada ya kuanza vita ya Mashariki ya Kati, kambi zilizopo nchini humo zimeshambuliwa mara kadhaa na Iran.
Wakizungumza na mitandao wa Dawn kwa sharti la kutotajwa majina, wanadiplomasia hao walisema umakini unahitajika kwa Pakistan ili kutofungamana na upande wowote.
‘’Ikiwa Pakistan itashindwa kukidhi matarajio ya Saudi Arabia wakati wa mgogoro ina hatari ya kupoteza uwekezaji, ufadhili wa kifedha,’’ walisema wanadiplomasia hao.
Wachambuzi hao walisema Pakistan inapaswa kuwa makini ikiwa ni pamoja na kupuuza baadhi ya makubaliano katika mikataba wa ulinzi wa kimkakati kati yake na Saudi Arabia wa SDMA.
‘’Pakistan inaweza kusaidia mahitaji ya ulinzi ya Saudi Arabia kupitia mafunzo na masuala mengine lakini kuna wanaosema haitakuwa sehemu ya mapambano la kijeshi ya Saudi Arabia na Iran. Hilo ni gumu kuthibitisha,’’ walidai.
Walibainisha kuwa mikataba huo wa mwaka 2025 ni kama uliifunga Pakistan kwa Saudi Arabia, hivyo si rahisi kwa Pakistan kutosaidia chochote.
‘’Hatari kwa Pakistan iko katika ukweli kwamba ahadi hii ya ulinzi iko juu ya utegemezi mkubwa zaidi wa kiuchumi. Saudi Arabia si mshirika tajiri tu, bali ni mmoja wa washirika wachache wa nje wanaoweza kuchangia uchumi wa Pakistan kwa kiasi kikubwa, hilo ndio linalotupa mashaka,’’ walisema.
Hata hivyo, maoni ya wanadiplomasia hao yalipingwa na mamkala nchini Pakistan zikibainisha kuwa ushirika wa nchi hiyo na Saudi Arabia umejikita zaidi kiuchumi na kwamba kinachoendelea ni mgogoro kati Iran na mataifa mengine.