Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanahabari kitanzini, utafiti waeleza suluhisho

Wakati wanahabari nchini Pakistan wakidai kuminywa katika utendaji wao wa kazi, Taasisi ya Utafiti, Utetezi na Maendeleo nchini humo (Irada) imetoa ripoti ya utafiti wake kuhusu kuboreshwa kwa mifumo ya sheria ili wanahabari wafanye shughuli zao kwa uhuru.

Utafiti huo wa kuanzia 2016 hadi 2024 umependekeza marekebisho ya Sheria ya Kuzuia Uhalifu wa Kielektroniki (PECA), ikieleza kuwa ndio inayotumika kukandamizi uhuru wa vyombo vya habari nchini Pakistan.

‘’Mwanahabari Ducky Bhai alikamatwa na kulazimishwa kukiri kosa ambalo hakulifanya.  Pia wapo Saadur Rehman na Ducky Bhai. Hawa pia walidai kunyanyaswa walipokamatwa na shirika la kitaifa la upelelezi wa uhalifu mtandaoni la Pakistan,’’ alisema mwanahabari Arshad Sharif wakati akihojiwa na mtandao wa Dawn.

Ripoti hiyo ya kurasa 230 inaonesha ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari.

‘’Kuna wanahabari 142 taarifa zao zilirekodiwa baada ya kubanwa na kushindwa kutekeleza majukumu yao. Ni ongezeko la karibu asilimia 60 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Punjab na Islamabad ziliibuka kama maeneo hatari zaidi.’’

‘’Kufungwa kwa mitandao ya simu na kufuatiliwa kwa makundi sogozi limekuwa jambo la kawaida pia,’’ inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imeainisha vifungu mbalimbali katika sheria iliyofanyiwa marekebisho ya PECA na kueleza kuwa ina vipengele vinavyominya uhuru wa kujieleza.

‘’Ingawa serikali inasisitiza kwamba sheria imeundwa kuwalinda raia kutokana na unyanyasaji mtandaoni na kauli za chuki, tuliozungumza nao wanasema sheria imejaa ukandamizaji na kunyamazisha sauti za wakosoaji,’’ inaeleza ripoti hiyo.

Mwanahabari Iqbal Khattak akihojiwa na mtandao wa Dawn kuhusu ripoti hiyo alisema, "sheria ni kikwazo kwa sababu kuna habari unajua wazi ukiripoti utakamatwa, kuwekwa kizuizini au mtandao yako ya kijamii kufungiwa.’’