Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yas yajivunia mbio za Selous Marathon

Dar es Salaam. Kampuni ya Mawasiliano ya Yas, inajivunia sehemu ya wadau wanaounga mkono mbio za TCB Selous Marathon, zinazojijengea nafasi ya jukwaa muhimu la kuhamasisha afya, kukuza utalii na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mkoani Morogoro, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ aliwapongeza waandaaji na wadau mbalimbali kwa kuunga mkono mbio hizo kutokana na kukuza michezo, afya, utalii na uchumi wa nchi.

“Serikali inaendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo kwa sababu ni nyenzo muhimu ya kujenga taifa lenye afya na nguvu kazi yenye tija, matukio haya yanasaidia pia kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii ndani na nje ya nchi,” alisema Mwinjuma.

Alitumia nafasi hiyo kwa kuwapongeza waandaaji wa TCB Selous Marathon na wadau kama Yas na Mixx kwa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii kupitia michezo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kusini, Joseph Mutalemwa alisema ushiriki wa kampuni hiyo katika mbio hizo unaakisi dhamira yake ya kuunga mkono mipango inayowaleta watanzania pamoja na kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Mutalemwa alisema mbio hizo zimekuwa zaidi ya mashindano ya riadha kwa kuwa inachangia kuitangaza Morogoro na vivutio vyake vya utalii, huku ikifungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi na wafanyabiashara wanaonufaika na shughuli zinazozunguka tukio hilo.

“Tunafurahia sehemu ya tukio hili ambalo sio tu linahamasisha afya na ustawi wa jamii, bali pia linasaidia kuitangaza Morogoro kama kitovu cha utalii na shughuli za kiuchumi, alisema Mutalemwa.

Alisema Yas na Mixx zinaamini michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga afya bora, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuhamasisha maendeleo endelevu katika jamii, ambapo itaendelea kuwekeza ili kuimarisha huduma za mawaliano.

Mutalemwa alisema kampuni hiyo kwa sasa ina zaidi ya minara 4,800 nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuhakikisha huduma bora za mawasiliano zinazopatikana katika maeneo mengi zaidi ya Tanzania.

“Sambamba na hilo huduma za kifedha za Mixx zinaendelea kuwawezesha Watanzania kufanya miamala kwa usalama, haraka na kwa urahisi, jambo linalochangia kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na matumizi ya huduma za kidijitali,” alisema.

Kwa upande mshiriki wa mbio hizo, Janeyah Mkwizu alisema TCB Selous Marathon imekuwa jukwaa muhimu linalowakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi huku ikihamasisha afya na kuitangaza Morogoro kama moja ya maeneo muhimu ya utalii nchini.

“Mbio hizi zimekuwa zaidi ya mashindano, zinatuleta pamoja kama jamii, zinatuhamasisha kuzingatia afya zetu na wakati huo huo zinaitangaza Morogoro, tunawashukuru wadau kama Yas na Mixx ambao wanaendelea kuunga mkono matukio kama haya yenye manufaa kwa jamii,” alisema Mkwizu.