Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbu kuipeperusha bendera ya Taifa, Marekani leo

Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu. Picha na Maktaba

Boston, Marekani. Bendera ya Taifa leo itakuwa inapeperuka katika mashindano makubwa ya riadha ya Boston Marathon 2026 yanayofanyika Boston, Marekani ambapo Tanzania inawakilishwa na Mwanariadha Alphonce Felix Simbu.

Ni mbio ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka zikishirikisha wanariadha wenye majina makubwa duniani wa mbio ndefu kutoka nchi tofauti.

Kwa mwaka huu zitakuwa zikifanyika kwa mara ya 129 tangu zilipoanzishwa na kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1897.

Boston Marathon ni miongoni mwa mashindano makubwa saba ya riadha duniani kutokana na thamani, zawadi kwa washindi na mvuto wake kwa wapenzi wa riadha duniani.


Historia ya Geay, Ikangaa

Katika mbio za leo, Simbu ambaye anaingia akiwa anajivunia rekodi yake ya kukimbia kwa saa 2:04:38 katika Mbio za Valencia Marathon, 2024 atakuwa na kibarua cha kufikia ama kuweka historia mpya zaidi ya ile iliyowekwa na Juma Ikangaa mwaka 1989 na Gabriel Geay mwaka 2023.

Wawili hao ndio Watanzania waliofanikiwa zaidi katika Boston Marathon ambapo kila mmoja alimaliza katika nafasi ya pili.

Mwaka 2023, Geay alizidiwa kete na Evans Chebet wa Kenya wakati mwaka 1989, Ikangaa alitanguliwa na Abebe Mekonnen ambaye aliibuka kinara.


Noti za kumwaga

Kwa kumaliza katika nafasi ya kwanza ama ya pili au ya tatu kwenye mashindano hayo, Simbu atajihakikishia kitita kikubwa cha fedha kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo.

Kiujumla waandaaji wa mbio hizo wametenga kiasi cha Dola 1.5 milioni (Sh3.9 bilioni) ambazo watazigawa kwa washindi mbalimbali upande wa wanawake na wanaume katika mbio ndefu pamoja na mbio za baiskeli za walemavu.

Katika mbio ndefu, mshindi ataondoka na kitita cha Dola 150,000 ((Sh389 milioni), mshindi wa pili atavuna Dola 75,000 (Sh195 milioni) na mshindi wa tatu ataondoka na Dola 40,000 (Sh104 milioni).

Kwa Mwanariadha ambaye atavunja rekodi katika mashindano hayo, atapata nyongeza ya Dola 50,000 (Sh130 milioni) katika zawadi yake.


Vita na vigogo

Hata hivyo Simbu atalazimika kufanya kazi ya ziada ili aweze kuondoka na kitita hciho cha fedha kwa kuibuka mshindi, mshindi wa pili au wa tatu kwenye mbio hizo za leo.

Hiyo ni kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya Wanariadha bora na wenye historia nzuri ya kushinda mbio tofauti duniani ambao nao leo watashiriki Boston Marathon.

Mshindi wa mbio hizo mwaka jana, John Korir ni miongoni mwa wanariadha ambao wamethibitisha kushiriki Boston Marathon leo huku pia akiwepo mshindi wa New York Marathon 2025, Benson Kipruto.

Nyota wengine ambao watashindana na Simbu kuwania vitita vya Boston Marathon ni Milkesa Mengesha, Cybrian Kotut, Abdi Nageeye, Lemi Berhanu, Hailemaryam Kiros, Alex Masai, Mohamed Esa na Tsegay Weldlibanos.