Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto: Semu amechora ramani ya mapambano Uchaguzi Mkuu

Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Muktasari:

  • Ingawa Zitto hakufafanua maana ya kuchora ramani, lakini kwa haraka ni namna Semu alivyotumia haki yake kujiondoa katika mbio za kuwania uteuzi wa urais baada ya ujio wa kada mpya, Luhaga Mpina aliyetokea CCM.

Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu amechora ramani ya namna chama chao kitakavyopambana katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Ingawa Zitto hakufafanua maana ya kuchora ramani, lakini kwa haraka ni namna Semu alivyotumia haki yake kujiondoa katika mbio za kuwania uteuzi wa urais baada ya ujio wa kada mpya Luhaga Mpina aliyetokea CCM.

Ingawa haikuwa rahisi kwa kiongozi kujiondoa katika mbio, hata hivyo ulitumika ushawishi mkubwa kutoka kwa viongozi waandamizi wa chama hicho kupitia vikao mbalimbali vilivyofanyika jana Jumanne Agosti 5, 2025.

 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu

Mapema leo Agosti 6, 2025 ACT Wazalendo kupitia kwa Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Shangwe Ayo alitoa taarifa kwa umma ikisema  Semu aliyetiania kuwania urais, kujitoa katika mchakato huo.

"Semu alieleza halmashauri kuu kuwa amechukua hatua hiyo, katika kutekeleza wajibu wake wa kiuongozi ili  kukiwezesha chama kutekeleza wajibu wa kimapambano ya kuiondosha CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa ya sasa nchini," amesema Shangwe.

Akitoa neno la shukrani baada ya viongozi wakuu kuhutubia, Zitto ambaye ni kiongozi mstaafu wa chama hicho, amesema Semu amekisaidia chama na Taifa na miezi mitatu ijayo itakwenda kuzibadili siasa za Tanzania.

"Tunakwenda kwenye miezi mitatu migumu sana, lakini ni miezi mitatu ya kurejesha heshima ya kura na kiongozi wetu wa chama ametuchorea tunakushukuru sana na Mungu akubariki."

"Utakumbukwa kama kiongozi ambaye uliyeweka pembeni matakwa yako, kwa ajili ya matakwa ya Taifa. Mmewaona watiania wa urais Tanzania (Mpina na Aaron Kalikawe) hii ni vita ya kizazi kitakwenda kumaliza kazi niliyoishinda," amesema Zitto.