Sakata la kupanda kwa bei ya vifurushi vya simu limetinga bungeni, ambapo Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amembana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akimtaka kueleza iwapo suala hilo ni utaratibu ama wizi.

Hatua hiyo imekuja leo Alhamis Novemba 10, 2022 wakati Waziri Nape wakichangia mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo pamoja na mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka 2023/24.