Uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam umesema upo mbioni kulifumua na kuliboresha eneo linalotumiwa na abiria wanaosafiri kwenda Zanzibar na kurudi Dar es Salaam (baggage room).

Maboresho hayo yatakayofanyika mwakani yamelenga kuweka mazingira mazuri ya miundombinu ya eneo hilo, pamoja na kuleta ufanisi kwa taasisi zinazotoa huduma eneo hilo.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo jana, katika mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusu mikakati ya taasisi yake, ikiwamo changamoto zinazoikumba ‘baggage room.’