Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku amekuwa ni Mtanzania wa kwanza na mwanamke wa kwanza kuiongoza kampuni hiyo kubwa nchini. Katika mahojiano maalum na Mwananchi, anaelezea safari yake hadi kufikia nafasi hiyo na mikakati yake ya kuipaisha Zaidi Vodacom katika shughuli zake za kuwaunganisha watanzania kupitia teknolojia ya mawasiliano na kuboresha maisha yao.