Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Desemba 22,2022 atawaongoza wageni 2,300 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kuzindua ufunguaji wa lango la handaki litakaloruhusu maji yaanze kujaa katika bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere liloanza kujengwa tangu mwaka 2019.