Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT wapinga kauli ya RC kuzuia kubandikwa mabango ya karatasi

Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo Omar Said Shaaban akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chama hicho Vuga Zanzibar. Picha na Jesse Mikofu

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha sheria ya uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 2018, vifaa vyote vinavyotakiwa kutumiwa na wagombea na ubandikaji wa mabango

Unguja. Chama cha ACT Wazalendo kwa mara nyingine, kimesema kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Mustapha Kitwana kupiga marufuku ubandikaji wa mabango ya makaratasi badala yake watumie mabango ya kidijitali ni batili.

Hivi karibuni, mkuu huyo wa mkoa wakati akizungumza na waandishi wa habari alisema katika mkoa huo hataruhusu kubandikwa mabango ya aina yoyote ya karatasi badala yake wanaotaka kufanya hivyo watumie mabango ya kidijitali kwa kile alichokitaja kuwa ni kuweka usafi wa mazingira.

Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kukosoa kauli Kitwana, ikiwamo ni pamoja na  aliyoitoa Aprili mwaka huu akiwataka wafanyakazi wote waliopo chini ya ofisi yake katika mkoa huo kuwasilisha kadi zao za mpiga kura katika ofisi yake ili zihakikiwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, 2025 mjini Unguja, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Omar Said Shaaban amesema kitendo hicho ni kuingilia majukumu ya Tume ya Uchaguzi kwani mabango hayo yapo kisheria kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2018.

“Hii tabia ya kuwa watu wanataka kuvunja sheria kwa sababu fulani, haikubaliki mpango wake ni batili na hautekelezeki na ni kwenda kinyume na sheria” amesema Shaaban.

Kifungu cha 64 cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2018 kinazungumzia vifaa vya kampeni na ubandikaji wa mabango kwamba Tume itatayarisha mwongozo wa uchapishaji na ubandikaji wa mabango ya wagombea na kutoa kwa wahusika.

Kwa mujibu wa kifungu cha 64 (2) vifaa vyote vinavyotakiwa kutumika wakati wa kampeni kwa vyama husika vitapaswa kuwasilishwa kwa Tume ya uchaguzi ivikague.

Hata hivyo amesema chama hicho kinawatoa hofu watu wote wenye nia ya kubandika mabango yao watafanya hivyo kwani sheria ipo inayotoa mwongozo huo na sio utashi wa viongozi fulani.

“Watu wasiwe na hofu hili halitafanyika na sheria hiyohiyo ya uchaguzi inasema mtu akibandua au kuchana mabango ya mgombea ni kosa la jinai,” amesema.

Pia, sheri hiyohiyo inasema mabango yatakayobandikwa kwenye maeneo mbalimbali yanatakiwa kubanduliwa siku 90 baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

Wakati huohuo ACT kimelaani kitendo cha vijana wajasiriamali waliodaiwa kukamatwa na kuteswa na askari wa Mji Mkongwe kwa madai ya kukiuka maelekezo ya kutofanya biashara katika eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea Juni 26, 2025 baada ya wajasiriamali 19 waliokuwa wakifanya biashara zao kudaiwa kukamatwa na kudaiwa kuteswa na kuumizwa na askari hao.

Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mkongwe, Ali Bakar kutoa ufafanuzi wa kadhia hiyo, amesema wanatarajia kutoa taarifa kwa umma kuhusu jambo hilo bila kufafanua zaidi na lini taarifa hiyo itatolewa

Shaaban amesema hakuna sheria inayoruhusu watu kuteswa hata kama wamekiuka sheria badala yake wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Amesema chama hicho kinakusudia kufanya mambo mawili, kwanza kuwasaidia vijana hao kuwashtaki waliowafanyia makosa hayo na pili kuushtaki mamlaka kutoka na ukiukwaji wa haki za binadamu

“Tutaiandikia Unesco (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni) barua kueleza madhila yanayotokea katika eneo la uhifadhi ikiwamo manyanayaso ili tujue kama inaruhusiwa kufanya hivyo.”

“Sisi hatupungi uhifadhi wa Mji Mkongwe bali tunachotaka ni sheria zifuatwe kama watu wanakosea basi washtakiwe sio kupigwa na kunyanyaswa,” amesema.