Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia aagiza kuondolewa vikwazo vinavyokwamisha haki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi akizungumza leo Jumamosi Juni 20, 2026 wakati wa uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika katika Viwanja vya Maonesho Kizimbani, Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Muktasari:

  • Ni katika uzinduzi wa kapeni ya kitaifa ya Msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid awamu ya pili ambayo inalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi na kushughulikia changamoto zilizopatikana awamu ya kwanza ikiwa ni pamoja na wananachi wengi kutofikiwa na umbali wa upatikanaji wa huduma.

Unguja. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid (MSLAC) imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na programu zote zilizowahi kufanyika za kisheria huku akiwataka viongozi kuodoa vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa haki.

Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu tangu ilipoanzishwa kampeni hiyo (2023-2026), wananchi zaidi ya milioni nne wamefikiwa na kampeni hiyo katika kusikiliza na kutua changamoto zao za kisheria.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Juni 20, 2026 katika hotuba yake iliyosomwa na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi alipomwakilishi wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid awamu ya pili (MSLAC II) katika viwanja vya Dole Unguja, Zanzibar.

“Ondoeni vikwazo vyote vinavyokwamisha haki. Hakikisheni mwananchi anapata huduma kwa heshima na kwa wakati, wajibikeni kwa matokeo na sio kwa taratibu pekee. Shirikianeni kufanikisha kampeni hii ya huduma za msaada wa kisheria,” amesema Rais Samia

Amesema kampeni hii imeimarisha ushirikiano kati ya taasisi za sheria, imeweka msingi wa mfumo wa kitaifa wa msaada wa kisheria, na wadau wengi wameingia katika utoaji wa huduma hizi za msaada wa kisheria.

“Hivyo, hujenga mfumo wa haki unaowafikia wananchi wote. Niwaombe wadau, hususan wadau wa maendeleo na taasisi binafsi, tuendelee kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwafikia wananchi wetu,” amesema.

Pia, Rais Samia amezitaka wizara zinazohusika zifanye kazi kwa karibu na wadau wote wanaohusika na mnyororo wa haki nchini huku utekelezaji wa kampeni uzingatie viwango vya kitaifa vya utoaji huduma, mfumo wa kupima utendaji, ufuatiliaji na tathmini, mfumo wa malalamiko na mrejesho kwa wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeze kwa wingi kupata huduma za msaada wa kisheria zitakazowezesha kupata ufumbuzi wa changamoto za kisheria zinazowakabili na kuwezesha kutumia muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli za kiuchumi zitakazowaletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Amesema Wizara ya Katiba na Sheria imeanzisha kituo cha huduma kwa mteja ambacho kinapokea na kushughulikia malalamiko, changamoto, na migogoro ya kisheria ya wananchi.

Pia, amesema Serikali imeunda mfumo wa kidijitali wa kuhakikisha uzingatiwaji wa matakwa ya kisheria kwa watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria, kupokea na kuchambua takwimu za msaada wa kisheria nchini.

Kuwezesha utaratibu wa kushughulikia changamoto za kisheria, ikiwemo rufaa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na kuwezesha wananchi kupata huduma za kisheria na mrejesho wa haraka juu ya masuala yao waliyoyawasilisha.

Kiongozi huyo wa kitaifa, ametaja sababu za kuamua kuwa na awamu ya pili ya kampeni hiyo ni kutokana na kubaini changamoto ikiwa ni pamoja na wananchi wengi kutofikiwa, umbali wa utoaji wa huduma na gharama kubwa hivyo kampeni hii uya wamu ya pili itakwenda kutatua changamoto hizo.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria,  Dk Juma Homera amesema kampeni ya awamu ya kwanza ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa ambapo walifikiwa watu zaidi ya 4.1 milioni kati ya hao, Tanzania Bara watu milioni 3.7 na Zanzobar 422,908.

Kwa mujibu wa Dk Homera katika kipindi hicho jumla la ya migogoro 26,876 ilipokewa kati ya hiyo migogoro zaidi ya 14,000 ilitatuliwa na mingine 12,000 inaendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi.

Amesema kati ya watu waliofikiwa wafungwa walikuwa 7574 ambao walikuwa na vizuizi mbalimbali huku matukio zaidi ya 50,000 ya kijamii yalisajiliwa.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Kesi na Uthibiti Ubora Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Camilius Ruhinda amesema ushiriki wao katika kampeni hiyo itarahisisha utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi.

“Tunaamini kwamba tutakaposhiriki zile changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wananchi, tutaweza kuzitolea maelezo ama kushauri ama kusaidia pale ambapo, wanapata mkwamo hususani katika kupata huduma zinazohusiana na masuala ya kisheria,” amesema.

Naye Wakili na Mwandishi wa sheria kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, Happyphania Luena amesema kwasasa ofisi hiyo inafaanya tafsiri mbalimbali za sheria na tayari imefanya tafsiri ya toleo la mwaka 2023 la kingereza kwenda kiswahili hivyo wananchi watanufaika kwa kusoma sheria hizo kwa lugha ya Kiswahili wanayoilewa vyema.

“Tunawakaribisha wananchi waje wapate uelewa wa sheria mbalimbali na kwasasa zimetafsriwa na kuwasaidia kauelewa katika lugha yao ya Kiswahili,” amesema.