Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanachama 453 wa ACT- Wazalendo watajwa kujiunga na CCM Pemba

Wanachama wa ACT Wazalendo wakikusanya kadi zao baada ya kuhamia CCM katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa Upande wa Pemba

Muktasari:

  • Wamepokewa katika uzinduzi wa mkutano wa kampeni za mgombea wa CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi kisiwani Pemba.

Unguja. Zaidi ya wanachama 450 wa chama cha ACT Wazalendo wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakieleza kuvutiwa na uongozi bora wa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Wanachama hao wamepokewa leo, Septemba 15, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Pemba katika Viwanja vya Gombani ya Kale, Mkoa wa Kusini Pemba.

Idadi ya wanachama hao imetajwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa, akisema wameamua kuunga mkono chama hicho kutokana na maendeleo yaliyofanyika.

Mwakilishi wa kundi hilo, aliyekuwa Mjumbe wa ngome ya ACT Wazalendo kutoka Micheweni, Faki Ali Juma, amesema wameamua kwa hiari yao kujiunga na CCM baada ya kushuhudia kasi ya maendeleo na dira ya uongozi wa Dk Mwinyi, akisisitiza kuwa chama hicho ndicho kinachoonesha mwelekeo wa kweli wa kuijenga Zanzibar.

“Tumevutiwa na uongozi wake, ndiyo maana tumeamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi,” amesema Faki.

Ameahidi kuwa watapiga kura nyingi ifikapo Oktoba 29 na kuhamasisha wengine wawapigie kura wagombea kutoka CCM.

Amesema kuwa wamejiwekea mkakati wa kuhakikisha wanahamasisha kila mmoja, wakiwemo wagombea wengine kutoka vyama vingine, kikiwemo chama walichotoka cha ACT.