Bana matumizi ya Serikali iangaliwe upya - Sigalla
Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla.
Muktasari:
Profesa Sigalla ametoa kauli hiyo ikiwa ni tathmini yake ya mwaka mmoja wa utawala wa Rais John Magufuli akisema amerejesha imani kwa wananchi kutokana na uchapakazi alioonyesha tangu aingie madarakani baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.
Dar es Salaam. Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla amesema hatua ya Serikali kubana matumizi ikiwamo kuzuia mikutano na semina inapaswa kuangaliwa upya kwa mwaka ujao wa fedha kwa sababu ndiyo itakayosaidia mzunguko wa fedha na hivyo wananchi wa chini kuwa na kipato cha uhakika.
Profesa Sigalla ametoa kauli hiyo ikiwa ni tathmini yake ya mwaka mmoja wa utawala wa Rais John Magufuli akisema amerejesha imani kwa wananchi kutokana na uchapakazi alioonyesha tangu aingie madarakani baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.
Baadhi ya mambo aliyofanya ni kudhibiti matumizi holela ya fedha kwa kuzuia semina na warsha kufanyika kwenye hoteli, kufuta posho za vikao na safari za nje zisizo na tija.