Masauni: Ajali za barabarani zimepungua nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo. Picha na Joyce Mmasi

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kabla ya mkakati kupunguza ajali hizo kulitokea vifo 467 na baada ya mkakati  vimetokea vifo 376.

Dar es Salaam. Tathmini ya miezi miwili iliyofaywa na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani inaonyesha kuwepo kwa upungufu wa ajali 106 ambazo ni sawa na asilimia 18 tofauti na ilivyokuwa awali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kabla ya mkakati kupunguza ajali hizo kulitokea vifo 467 na baada ya mkakati  vimetokea vifo 376.

Habari zinazohusiana

Waziri Masauni amesema katika kipindi hicho kumekuwa na upungufu wa ajali na vifo na majeruhi yaliyotokana na pikipiki ambapo kabla ya mkakati kulitokea  ajali 200 na vifo 118 lakini baada ya mkakati zimetokea ajali 170 na vifo 124.

Waziri amewataka madereva na wamiliki wa vyombo vya moto na watu miaka wote wa barabarani kuzingatia sheria za usalama barabarani sheria za usafirishaji na kanuni zake wakati wanapotumia barabara.