Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PM ataka wazazi kuwaeleza watoto madhara ya ‘unga’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa .. Picha na Emmanuel Herman

Muktasari:

  • Majaliwa ametoa wito huo leo (Alhamisi) mjini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya yaliyofanyika kitaifa mjini hapa.
  • Majaliwa amesema kuwa Serikali iko kwenye malengo yake ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda hivyo kama Taifa hawatawaacha vijana ambao ndiyo walengwa wakubwa wa kuinua Taifa kiuchumi wakipotea katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo vita yake imeshatangazwa.

Dodoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi nchini kuwa na muda wa kukaa na watoto wao na kuwaeleza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya  kwani wao ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

Majaliwa ametoa wito huo leo (Alhamisi) mjini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya yaliyofanyika kitaifa mjini hapa.

Majaliwa amesema kuwa Serikali iko kwenye malengo yake ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda hivyo kama Taifa hawatawaacha vijana ambao ndiyo walengwa wakubwa wa kuinua Taifa kiuchumi wakipotea katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo vita yake imeshatangazwa.

Amesema vita ya dawa za kulevya inaanzia kwenye ngazi ya familia hivyo ni wajibu wa kila mzazi kukaa na watoto wake ili kuwaeleza madhara ya natumizi hayo ili wajiingize huko.

"Wazazi na walezi wakae na watoto wao na pia waseme na watoto wa majirani zao kwa sababu ukiwaacha watoto wa majirani zako waharibike ni wazi kuwa wanaweza kuwaharibu na watoto wako," amesema Majaliwa.