Polisi waliomdhalilisha mchungaji wakufuzwa kazi

Muktasari:

Polisi hao, walidaiwa kumkamata mchungaji huyo na mwanamume mwingine katika nyumba moja ya kulala wageni wilayani Hai, kumshurutisha avue nguo, kumpiga picha na kudai awalipe Sh10 milioni.

Moshi. Askari Polisi wanne mkoani Kilimanjaro, waliotuhumiwa kumtengenezea tukio la ushoga mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamefukuzwa kazi.

Polisi hao, walidaiwa kumkamata mchungaji huyo na mwanamume mwingine katika nyumba moja ya kulala wageni wilayani Hai, kumshurutisha avue nguo, kumpiga picha na kudai awalipe Sh10 milioni.

Hata hivyo, mchungaji huyo ambaye jina lake tunalihifadhi, aliwalipa Sh5.4 milioni na polisi hao kumwachia baada ya kumshikilia kwa saa sita.

Habarii zaidi soma Gazeti Mwananchi