Rais Magufuli awatunukukia kamisheni maofisa 422 wa JWTZ

Muktasari:

  • Kabla ya kutunuku kamisheni hizo Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima lililondaliwa na maofisa hao.

Rais John Magufuli leo Jumamosi amewatunukia kamisheni ya luteni usu kwa maofisa 422 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania(JWTZ), katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kabla ya kutunuku kamisheni hizo Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima lililondaliwa na maofisa hao.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli alikabidhi zawadi kwa maofisa waliofanya vizuri wakati wa mafunzo hayo wakiongozwa na Hamis Mwanitega aliyetajwa kufanya vizuri zaidi kuliko wote.

Maofisa wengine waliopata zawadi ni Haji Kimaro aliyefanya vizuri darasani, John Mkua aliongoza kwenye mafunzo kwa vitendo huku Donatia Kimario akiibuka kidedea miongoni mwa wanawake walioshiriki kwenye mafunzo hayo.

Upande wa kikosi cha ubaharia Ally Kitawala aliibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi kwenye kikosi hicho.

Katika kundi la marubani wa ndege vita waliofanya vizuri ni Hamza Msuya na Albert Fanuel.