Trafiki auawa Kibiti, gari lao lachomwa moto
Muktasari:
Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa gari la askari hao pia limechomwa moto na kwa sasa vikosi vya ulinzi na usalama vinaelekea eneo la tukio.
Pwani. Watu wasiojulikana wamemuua askari wa Usalama Barabarani katika Kijiji cha Bungu B wilayani Kibiti, mchana huu.
Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa gari la askari hao pia limechomwa moto na kwa sasa vikosi vya ulinzi na usalama vinaelekea eneo la tukio.
Tutaendelea kukujuza jina la askari huyo na namna mauaji hayo yalivyotokea hivi punde.