VIDEO-Lema, Nassari, Msigwa waingia Takukuru

Muktasari:

Wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai unaonyesha wa jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa

Wabunge wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai unaonyesha wa jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa.

Wabunge wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa leo Jumatatu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.

Wabunge hao wamewasili katika ofisi hizo saa 8.39 mchana na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri.

Katika kile ambacho waandishi hawakukifikiria, wabunge hao waliwasili kwa miguu na kuelekea moja kwa moja ndani ambapo waandishi walizuiwa kuingia.

Ushahidi huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha  kueleza jinsi madiwani wao walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.