Wasimamizi wa Ukuta wa Chadema watangazwa

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Muktasari:

Mbowe ameitaja mikakati hiyo ikiwamo kamati za kuhamasisha Ukuta.

Dar es Salaam na Arusha. Chadema imetangaza safu yao ya kutoa elimu ya maandamano ya Ukuta.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  ametangaza mkakati wa chama hicho kufanikisha mikutano na maandamano  ya walichokiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), huku jeshi la polisi nalo likijiandaa kukabiliana nao.

Mbowe ameitaja mikakati hiyo ikiwamo kamati za kuhamasisha Ukuta.