Ajibu aibeba Simba Taifa, Bandari yakubali kipigo

Saturday October 12 2019

 

By CHARITY JAMES

KIKOSI cha Simba kimeonyesha uwezo kipindi cha pili kwa kuliandama zaidi lango la wapinzani wao Bandari FC na endapo wangeanza hivyo kipindi cha kwanza wangepata mabao mengi zaidi.
Simba wamepata bao 1-0 kupitia kwa Ibarahim Ajibu ambaye alikwamisha mpira nyavuni akipokea pasi kutoka kwa Rashid Juma.
Kipindi cha pili Bandari  walizidiwa na kushindwa kupata nafasi ya kumpita beki Yusuph Mlipili aliyeingia kuchukua nafasi ya Joseph Peater ambaye alipewa nafasi ya kucheza akitoka kikosi cha Simba B.
Kukosa kwake uzoefu kulikuwa kunawapa nafasi wapinzani wao ya kupita upande wake kulishambulia lango la Simba ambalo lilikuwa na ngome imara kuanzia ulinzi hadi kipa.
Pamoja na kukosa mbinu za kupita pembeni Bandari walionekana kuimarika hasa eneo la kiungo ambapa hawakumpa uhuru Shariff Shiboub wa kupiga pasi kama alivyozoeleka.

Advertisement