Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya kufungwa na Brazil, Messi agoma kutundika daruga

Muktasari:

Argentina iliboronga tena katika michuano ya kimataifa jana baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 mbele ya wenyeji Brazil na kuondolewa katika nusu fainali ya michuano ya soka ya Copa America.

Lionel Messi ameahidi kuendelea kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina licha kushindwa tena kuiongoza kutwaa ubingwa wa soka wa Amerika Kusini jana Jumanne baada ya kufungwa mabao 2-0 na mahasimu wao wakubwa, Brazil katika mechi ya nusu fainali.

Nyota huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 32, ambaye alitangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya Argentina kufungwa katika fainali ya michuano hiyo ya Copa Amerika mwaka 2016, amesema hana mpango wa kutundika daruga baada ya kipigo cha jana.

"Kama naweza kusaidia kwa njia yoyote, nitaendelea kufanya hivyo. Najisikia vizuri sana kwenye kundi hili," alisema Messi ambaye ameshashinda mara tano tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia ya Ballon d'Or (Mpira wa Dhahabu).

"Hiki ni (kukosi) kizuri, kizazi cha wachezaji wenye talanta ambao wanaonyesha kwamba wanaipenda timu ya taifa.

"Matarajio ya baadaye ni makubwa na wana msingi mzuri, wanachohitaji na kupewa muda."

Messi atapata tena fursa ya kuondokana na balaa lake kwenye mashindano hayo mwakani wakati yatakapofanyika Argentina na Colombia, huku fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zikikaribia.

Katika hatua nyingine, kocha wa Argentina, Lionel Scaloni amesisitiza kuwa timu yake, ambayo ina wachezaji wapya wengi, ina dalili za kufanya vizuri baadaye licha ya kufungwa jana.

"Bila ya shaka, leo tulionyesha kuwa kundi hili linapenda jezi hii kuliko mtu mwingine yeyote," alisema kocha huyo.

"Tulionyesha pia ya timu hii ya baadaye ikiwa na wachezaji hawa na njia nzuri ya kufikia.

"Kucheza kwenye uwanja huu na hali hii na kuwa timu bora kwa wapinzani wetu.

"Haijalishi kwamba (Brazil) wanakwenda fainali, lakini kama tunajua tulichofanya leo, basi ni kuwa na matumaini."

Hata hivyo, alisema kipigo chao hakikuwa cha haki kwa sababu "hakuna timu nyingine yoyote iliyotengeneza nafasi nyingi za kufunga dhidi ya Brazil kama sisi".

Nafasi safi kwa Messi ilipatikana katika dakika ya 57 wakati mpira wa juu aliuoupiga uliupogonga besela. Scaloni alisema mkongwe huyo ndiye aliyeonekana chachu ya timu.

"Mara zote Brazil ilikuwa ikijaribu kuzuia pasi kumfikia na wakati wote tulikuwa tunamtafuta ili tumpe mipira," alisema Scaloni.

"Ilikuwa inafurahisha kumuona akicheza. (Mipango) Haikufanikiwa leo, lakini atapata nafasi nyingine na timu nzima pia."