KMC yaondolewa kimataifa, yafungwa nyumbani

Friday August 23 2019

 

By Oliver Albert

KMC imekuwa timu ya Kwanza ya Tanzania kuondolewa kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kuchapwa mabao 2-1 na AS Kigali ya Rwanda.
Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika  uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, KMC itabidi ijilaumu kwa kiwanho chake kibovu kilichopelekea kupata matokeo hayo.
Mabao ya AS Kigali katika mchezo wa leo yamefungwa na Rashid Kalisa na Erick Nsabimana wakati la KMC limefungwa na Yusuph Ndikumana kwa penalti.
KMC  ambayo ni mara ya kwanza inashiriki mashindano hayo, ilicheza vibaya hasa  eneo la ulinzi na ushambuliaji na kuwaacha wapinzani wao AS Kigali wakitawala Kama wako nyumbani.
Sasa KMC inarejea kwenye Ligi Kuu Bara iliyoanza kesho Jumamosi wakisubiri kuvana na Azam siku ya Jumanne ijayo.

Advertisement