Kagere afunika mkutano mkuu wa Simba

Sunday December 8 2019

 

By Imani Makongoro na Thobias Sebastian

Dar es Salaam.Mshambualiji Medie Kagere ni nyota pekee wa Simba aliyeshangiliwa na wanachama wa klabu hiyo katika mkutano mkuu wa klabu unaoendelea Dar es Salaam.

Katika mkutano huo ulioudhuliwa pia na wachezaji wa Simba, Kagere ndiye alikuwa kivutio.

Wachezaji hao waliwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere saa 4:20 na walipokuwa wakiingia ukumbini wanachama wa Simba waliwashangilia kwa kuwapigia makofi huku baadhi yao wakilitaja jina la Kagere ambaye wakati huo alikuwa akisalimiana na Salim Abdallah 'Try Again'.

Mshambuliaji huyo raia wa Rwanda alijua mashabiki wanahitaji nini, wakati wachezaji wengine wakikaa kwenye viti, Kagere alisimama na kuwapungia mikono mashabiki kwa ishara ya kusalimia kitendo kilichofanya azidi kushangiliwa kwa nguvu.

Advertisement