Kawhi ang'ara NBA All-Star Game

Muktasari:

Mechi hiyo ilitumika pia kumuenzi nyota wa zamani wa Los Angeles Lakers, Kobe Bryant aliyefariki kwa ajali ya helikopta, huku Team LeBron ikishinda.

Kawhi Leonard jana ameng'ara na Magic Johnson, ambaye yumo katika makumbusho ya wachezaji nyota (Hall of Fame), alivutia watu katika sherehe iliyofanyika kabla ya mchezo wa wachezaji nyota (All Star Game) wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA), katika usiku uliotumika kumuenzi marehemu Kobe Bryant.
Mtoto wa nyota huyo kipenzi wa timu ya Chicago, Anthony Davis alifunga mrusho mmoja kati ya mitatu ya adhabu kunogesha robo ya mwisho ya mchezo huo iliyokuwa ya kuvutia na timu ya LeBron ikashinda kwa pointi 157-155 dhidi ya timu ya Giannis.
Leonard alimaliza mchezo huo akiwa amefunga pointi 30 na kuokoa rebound saba na akazawadiwa tuzo ya mpya ya Kobe Bryant MVP. Zawadi hiyo imepewa jina la nyota huyo wa zamani wa Los Angeles Lakers, ambaye alifariki dunia katika ajali ya helikopta akiwa na binti yake Gigi na watu wengine saba wiki tatu zilizopita.
"Nataka kumshukuru Kobe kwa kila kitu alichonifanyia, mazungumzo yote ya muda mrefu na mazoezi. Asante sana," alisema Leonard, ambaye alikulia Riverside, California mashariki ya Los Angeles.
Giannis Antetokounmpo alimaliza mchezo huo akiwa amefunga pointi 25 na kunyakua rebound 11 na kuiongoza Team Giannis ambayo iliikalia kooni Team LeBron hadi dakika hizo za mwisho.
"Walikuwa wakikimbia na kurudi haraka nyuma kuzuia," alisema Leonard akizungumzia mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa tofauti na mchezo wa Ijumaa uliohusisha wachezaji wanaoinukia na kufunikwa na mashindano ya kudunk.
Huku zikiwa zimefungana pointi 156-155, na kanuni za mashindano zikieleza kuwa mshindi ni yule atakayekuwa wa kwanza kufikisha pointi 157, Davis alikwenda mstarini baada ya kuchezewa rafu na Kyle Lowry wa Team Giannis.
"Niliwaambia wachezaji wenzangu kuwa ningekosa mrusho wa kwanza na kujiambia kuwa ni lazima nifunge wa pili," alisema Davis, ambaye alikulia Chicago.
Na ndicho alichofanya na kumaliza mchezo ambao ulianza kwa mchezaji mwingine wa zamani wa Lakers, Johnson kutoa hotuba yenye hisia ya kumuenzi Bryant mbele ya mashabiki 20,900 katika uwanja wa United Center jijini Chicago.
"Hatutamuona tena mchezaji mwingine wa mpira wa kikapu kama Kobe," alisema Johnson, ambaye pia alitoa heshima kwa David Stern, kamishna wa NBA aliyefariki.
"Kufunga pointi 81 katika mechi moja. Kufunga pointi 60 katika mchezo wake wa mwisho. Na pia kutwaa ubingwa w aNBA mara tano."
James alifikia rekodi ya Kobe ya kupangwa mara ya 16 katika kikosi kinachoanza mechi ya NBA All Star Game. Bryant anashikilia rekodi ya kutwaa tuzo ya MVP mara nne.