Simba yawajaza mapesa mama lishe Mwanza

Thursday September 20 2018

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Ukiachana na wafanyabiashara wa vifaa vya michezo hususani jezi za timu za Simba na Yanga kuendelea kupiga pesa,  Mamantilie nao hawako nyuma, wanazidi kuingiza 'noti' za maana  kuelekea mpambano huo.

Milango bado haijafunguliwa, lakini wadau wameanza kumiminika kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mamantilie wameonekana kujipatia pesa hizo kwa wawateja mashabiki wanaopita kwenye migahawa yao kwa ajili ya kupata chochote na kutuliza njaa.

Sehemu kubwa ya mashabiki tayari wameanza kutiririka uwanjani hapo ili kushuhudia mpambano huo.

Advertisement