TFF yasogeza mbele uchaguzi Bodi ya Ligi

Monday October 21 2019

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake cha Oktoba 19, 2019 pamoja na mambo mengine imeongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za uchaguzi mdogo wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).

Sababu kubwa inayotajwa kwa kusogezwa muda mbele ni kutokana na muitikio mdogo kwa wagombea waliojitokeza kuchukua fomu hizo.

Uamuzi ya kusogeza muda mbele yamezingatia kanuni ya 10(6) ya kanuni za uchaguzi toleo la mwaka 2013.

Sehemu mojawapo ambayo inagombewa ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, baada ya aliyekuwa anashika nafasi hiyo Boniface Wambura mkataba wake kumalizika.

Utoaji wa fomu uliaanza leo Oktoba 21 mpaka Jumatano Oktoba 23, 2019 saa 10:00 jioni.

Advertisement