Bi Cheka azikwa Dar

Friday November 29 2019

 

By RHOBI CHACHA

MTOTO wa marehemu Bi Cheka, Kombo Shabani  amesema toka mama yake aanze kuumwa wasanii Chamuso na Shilole ndio waliowahi kwenda kumuona .
Akizungumza  na MCL Digital, Kombo amesema, mama yake kabla hajafariki alikuwa na ugonjwa wa kuanguka anguka na hii ilitokea mwaka jana mwishoni baada ya kufariki mtoto wake wa kwanza Yakub aliyekuwa anaishi Uingereza .
Kombo amesema, mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu mama yake alianguka chooni na kuugua kwa muda mfupi hapo ndio Shilole aliwahi kwenda kumuona, alianguka mara ya pili Meneja wa Aslay, Chambuso alienda kumjulia hali na baada ya hapo Chambuso ndio mtu pekee aliyekuwa anaenda mara kwa mara na hata kutoa msaada.
"Kiukweli toka mama aanze kuumwa Shilole alikuja mara moja kumuona alivyoanguka chooni mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu, Chambuso alikuwa anajitahidi sana kuja kumuona mama, zaidi ya hapo sikuwahi kumuona msanii mwingine ,kipindi yuko hai mama alikuwa anaanguka anguka alianguka mara mbili kwa mwaka huu, huu ugonjwa aliupata alipofariki tu mtoto wake wa kwanza Yakub aliyekuwa anaishi Uingereza "alisema Kombo
Aidha MCL Digital ilimuuliza Kombo, kuhusu wasanii aliofanya nao kazi Bi Cheka enzi za uhai wake ambao ni Amani James ' Mh Temba' na Said Fella 'Mkubwa Fella' kama waliwahi kwenda kumjulia hali Bi Cheka wakati anaumwa au hata alipoanza kuumwa ambapo alisema hawajawahi kufika.
"Hapana kwa kweli Temba hajawahi kufika hata siku moja, na hata Mkubwa Fella hajawahi kufika wala kupiga simu, huenda wako bize na majukumu mengine "alisema Kombo
Hata hivyo MCL Digital lilizungumza na Mheshimiwa Temba kwa njia ya simu kumuuliza juu ya habari hizi, alikiri kutokwenda kumuona Bi Cheka akiwa anaumwa kwani alikuwa mkoani.
"Ni kweli sikuwahi kwenda kumuona Bi. Cheka pindi anaumwa, japo taarifa ya kuumwa nilikuwa nayo, wakati anaumwa nilikuwa mkoani ila niliongea nae kwenye simu alinipigia dada mmoja akasema niongee na Bi. Cheka, niliongea nae na kumwambia nikirudi nitaenda ila sikwenda hiyo ilikuwa miezi mitano iliyopita "alisema Mh Temba
Kwa Upande wa Mkubwa Fella alipoulizwa na MCL Digital, alisema yuko kwenye kikao chamsingi azikwe salama.

Advertisement