Chris Brown aibuka kwa Vanessa Mdee

Saturday July 13 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Inawezekana kuna kitu kinapikwa kati ya mwanamuziki wa Marekani, Chris Brown na wanamuziki wa barani Afrika.

Baada ya kutangaza hivi karibuni kuwa ataachia wimbo na mwanamuziki wa nchini Nigeria, Davido, Brown amemfollow staa wa muziki Bongo nchini Tanzania, Vanessa Mdee maarufu  V. Money katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mkali huyo wa wimbo ‘Back To Love’ Brown   kamfollow Vanessa Mdee kwenye Instagram yake ambayo ina watu  wachache wasiozidi 3,000 anaowafuatilia.

Kupitia ukurasa wake Instagram Brown aliweka picha ya katuni inayoonyesha sura yake na Davido zikiwa zimevaa kofia za wapishi.

 “Inakuja hivi karibuni, ”aliandika chini ya picha hiyo.

Miongoni mwa watu waliotoa maoni yao ni  Vanessa aliyeweka alama ya moto kuashiria mambo ni moto huku Davido akisema “Ngoma kali.”

Advertisement

Advertisement