Corona yakatisha shoo za Diamond barani Ulaya

Friday March 13 2020

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mataifa mbalimbali barani Ulaya kumekatisha shoo za muziki za msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Diamond alikuwa na shoo katika nchi mbalimbali barani humo lakini kutokana na baadhi ya nchi hizo kukumbwa na ugonjwa huo, hataweza kufanya shoo yoyote.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameeleza kusitishwa kwa shoo hizo na kwamba zitapangwa tena baadaye.

Kutokana na tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo mataifa mengi yamezuia mikusanyiko ya watu.

Mbali na Ubelgiji, Diamond alipanga kufanya shoo Ufaransa, Ujerumani,  Finland na Sweden.

Advertisement