Dada Kanumba amzungumzia ‘mke’ wa Seth

Monday December 9 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Tina, dada wa aliyekuwa nyota wa filamu nchini Tanzania marehemu Steven Kanumba amesema mdogo wake Seth Bosco aliyefariki dunia Desemba 6, 2019 hakuwa na mke na ameacha watoto wawili.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 9, 2019 siku moja baada msichana aliyejitambulisha kwa majina ya Doris Mrema kusema ni mke wa Bosco.

Akizungumza na Mwananchi, Tina amesema hadi Bosco anafariki dunia hakuwa na mke, ana watoto wawili waliokuwa wanatambuliwa na familia.

Juzi Desemba 7, 2019 Doris alilieleza Mwananchi kuwa amekuwa na uhusiano na Bosco kwa miaka tisa na walikuwa wakiishi pamoja Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Amesema Bosco alipoanza kuumwa alirudi nyumbani kwao Mbezi Temboni hadi alipofariki dunia, kwamba walijaaliwa kupata mtoto mmoja na Bosco.

Advertisement